Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MALIMA AKEMEA VIKALI UNYANYASAJI WATU WENYE ULEMAVU

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Furaha Matondo wa tano katika mstari wa juu akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa CCM na watu wenye ulemavu mara baada ya kukabidhi msaada wa viti mwendo na fimbo nyuepe.

*******************

Na Sheila Katikula,Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima, amewataka wananchi kuacha kuwanyanyasa watu wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kosa na ikibainika hatua kali zitachululiwa ili kukomesha vitendo hivyo.

Hayo ameyasema jana kwenye hafla ya kukabidhi vifaa maalum kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalum Furaha Matondo iliwakutanisha wadau mbalimbali na viongozi wa Serikali na chama.

Amesema kila mtu anawajibu wa kuwathamini na kuwapenda watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada.

"Ninamshukru Mbunge wa viti maalum Furaha Matondo ambaye ameona umuhimu wa watu wenye ulemavu kwa kutoa msaada wa viti mwendo na fimbo nyeupe ambazo zitawasaidia wenzetu kufanya kazi zao kwa uharisi.

"Nawaomba tuwe na moyo wa upendo na tuone umuhimu wa watu wenye ulemavu kwani wanahitaji kupewa misaada mbalimbali kufanya hivi ni kitendo cha busara na kila mtu anapaswa kufanya hivi kama alivyofanya Mbunge.

Naye Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mwanza,Furaha Matondo amesema lengo la kutoa vifaa hivyo nikuwashika mkono ili waweze kufanya kazi zao kwa urahisi.

"Nimetowa msaada huu kwa lengo la kusaidia jamii yenye mahitaji maalum ili waweze kufanya kazi zao bila kupata changamoto.

Post a Comment

0 Comments