Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa ambayo yatafanyika kupitia wiki ya JKT itakayoanza tarehe 01 Julai 2023 hadi tarehe 09 Julai 2023. Tarehe 10 Julai 2023, itakuwa ndio siku ya Kilele cha Maadhimisho hayo, ambapo JKT limejipanga kufanya Maadhimisho hayo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, kwa kufanya Gwaride Rasmi, Maonesho ya Vikundi vya Sanaa na Utamaduni pamoja na bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT, Vikosi, Shule na Vyuo vya Ufundi Stadi vya JKT. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments