MBUNGE wa Jimbo la Amani Mhe.Abdul Yussuf Maalim na Mwakilishi wa Jimbo hilo Rukia Omar Mapuri pamoja na madiwani wa wadi za jimbo hilo wakikabidhi jezi kwa timu za jimbo hilo.
MBUNGE wa Jimbo la Amani Mhe.Abdul Yussuf Maalim akizungumza na wananchi wa jimbo hilo(hawapo pichani) katika ziara yake ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
MBUNGE wa Jimbo la Amani Mhe.Abdul Yussuf Maalim na Mwakilishi wa Jimbo hilo Rukia Omar Mapuri pamoja na madiwani wa wadi za jimbo hilo, wakikabidhi mabati ya kuezeka Maskani ya CCM ya Mjengoni iliyopo Banda la Mkaa Amani.
******************
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
WAZAZI na walezi nchini wameshauriwa kusimamia kikamilifu watoto wao wasome elimu ya dini ili wakue wakiwa na maadili mema.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Amani Mhe.Abdul Yussuf Maalim, katika mwendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Alisema watoto wanatakiwa kusimamiwa na kuwa karibu nao sambamba na kuwajengea mazingira rafiki ya kusoma vyuo vya madrasa mbali mbali ili wapate elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku.
Mhe.Abdul, aliwapongeza walimu wa madrasa mbali mbali katika jimbo hilo kwa kazi kubwa ya kuwalea na kuwajenga kiimani watoto mbali mbali ambao ndio watakaokuwa viongozi na walimu wa baadae.
Alielea kwamba katika uongozi wake atasimamia kikamilifu ustawi na maslahi ya walimu hao ambao wamekuwa wakiwekwa pembezoni bila kujali thamani ya elimu wanayotoa kwa jamii.
“Leo nimeona nije kukutembeleeni na kuleta sadaka kwa ajili ya ujenzi wa madrasa zetu zenye changamoto mbali mbali ili vijana wetu wapate elimu wakiwa katika mazingira mazuri”,. Alisema Mbunge huyo Abdul, wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa madrasa ya Tanbihil-ghafilyn.
Mbunge huo alisema lengo la ziara hiyo ni kuwapelekea wananchi huduma za maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Naye Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe.Rukia Mapuri, alisema wanaendelea kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi ili kufikia malengo ya kumaliza changamoto hizo.
Katika maelezo yake Mwakilishi huyo aliwataka wananchi hao kuhakikisha vifaa na walivyopewa wanavitunza vizuri na kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Wananchi wenzangu changamoto jimboni ni nyingi hivyo na sisi tunazitatua kwa awamu ambapo kila eneo lenye changamoto tutazitafutia ufumbuzi wake.”,alifafanua Mwakilishi huyo.
Naye Diwani wa Wadi ya Amani Makame Khamis Ame,aliwataka vijana kujiepusha na vitendo matumizi ya dawa za kulevya pamoja na wizi.
Alisema kuwa baadhi ya vijana waliojiingiza katika vitendo hivyo wameishia kupata matatizo ya akili na wengine kutumikia vifungo vya miaka mingi katika vyuo vya mafunzo nchini.
Kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Kilimahewa Akida Juma Makame, amewasihi wananchi kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Katika ziara hiyo alitoa vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa madrassa,amekabidhi jezi kwa timu mbali mbali na kukabidhi king’amuzi na dishi la Azam kwa Maskani ya CCM ya Machicha iliyopo Shehia ya Kwa Wazee.
0 Comments