*********************
Na Magrethy Katengu
Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kwa kushirikiana na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACRT) na Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania (EAFEO) ikiungana na Taasisi zote za Duniani kupitia Shirikisho la Taasisi za Kihandisi la Afrika Mashariki (EAFEO) na Shirikisho la Taasisi za Kihandisi la Afrika (FAEO) inataraji kuadhimisha Siku ya Uhandisi Duniani kwa Maendeleo endelevu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam rais wa Taasisi (IET) Mhandisi Dkt Gemma Modu amesema Maadhimisho hayo yatafanyika Machi 4 Mwaka huu Katika Ukumbi Kareemjee Jijini Dar es salaam yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo "Ubunifu wa Uhandisi kwa unaostahili zaidi " hiyo ni Kwa kuzingatia kuwa Dunia ipo zama za utandawazi ya Karne ya 21 na utashi kwenye Uchumi na Jamii zinazoendeshwa kwa nguvu ya Teknolojia ambayo Maendeleo yake ni makubwa na ya kasi .
"Madhumini ya siku hii ni kutoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa Uhandisi na watekelezaji wa kazi za Kiuhandisi wakiwamo Wahandisi na Mafundi wote katika kuleta Maendeleo endelevu ya Taifa letu kwa ujumla na kuboresha uelewa wa Umma kuhusu jinsi uhandisi wa Teknolojia ilivyo na umuhimu Kwa maisha yetu ya kila siku katika ulimwengu wetu wa Sasa"amesema rais Gemma
Aidha Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Washiriki zaidi ya 200 kutoka taasisi mbalimbali za Umma na binafsi zitapata fursa ya kuonyesha bunifu zao katika kutekeleza Miradi ya kimkakati inayoendelea nchini huku wanafunzi wa vyuo na Sekondari watashiriki na kuonesha bunifu zao za masomo yao .
0 Comments