Ticker

6/recent/ticker-posts

KANISA LA KATOLI KUFANYA MBIO ZA HISANI MARATHONI MEI 27 MWAKA HUU



**************

Na Magrethy Katengu

ASKOFU Mkuu Jimbo kuu la Dar es salaam Jude Rwa'ichi ameshauri Jamii kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha Afya zao .

Ushauri huo ameutoa Leo Jijini wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya Mbio za hisani za Pungu Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Mei 27 mwaka huu ikiwa na lengo la kukusanya kiasi cha fedha sh milioni 400 zitakazosaidia kuendeleza kituo cha Hija cha Pungu chenye historia ndefu ya Umishenari na Ukombozi wa Taifa hili.

Sanjari na hayo amesema Mbio hizo zitakuwa za aina nne Matembezi ya Kilometa 2,5 ambapo ada ya ushiriki ni Tsh 20000/=Mbio fupi za Kilometa 10,21 ada ya Ushiriki Tsh 30000/= atakayehitaji kushiriki atatakiwa kuingia mtandaoni kujisajili

Hata hivyo Askofu amesema fedha hizo zitakazotolewa itakuwa chachu kukarabati nyumba ya kumbukumbu ya Hayati Julius Kambarage Nyerere iliyopo pale Pungu ambapo kwa sasa ina hali mbaya na kujenga shule hiyo kusaidia kueneza Imani ya Romani Katoliki.

Aidha wito umetolewa wadau wa michezo wa riadha kujitoleza kwa wingi kushiriki mbio hizo Mashirika,Makampuni,Wafanyabiashara na Wadau wengine kufadhili kufanikisha lengo kuu

“Mbio hizi zitafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 27 Mei 2023 kuanzia saa 12 asubuhi,” amesema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Post a Comment

0 Comments