Ticker

6/recent/ticker-posts

ELIMU YA MAGONJWA ADIMU YAHITAJI KWENYE JAMII

Mwenyekiti wa Taasisi ya Malcom Bi.Sarah Chande akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 28,2023, katika Siku ya maadhimisho ya Magonjwa Adimu duniani ambapo huadhimishwa mwishoni mwa Mwezi Februari.Mwanzilishi wa Taasisi ya Ali Kimara,Bi.Sharifa Mbarak akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 28,2023, katika Siku ya maadhimisho ya Magonjwa Adimu duniani ambapo huadhimishwa mwishoni mwa Mwezi Februari.

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussen Mwinyi amesema Serikali itahakisha inawekeza madhubuti ili kuweza kutoa misaada inayohitajika kuwasaidia Watoto Wenye Magonjwa Adimu Ikiwepo Upatikanaji Oksijeni bure.

Ameyasema hayo jana Februari 28,2023 akiongea kwa njia ya simu katika Siku ya Maadhimisho ya Magonjwa Adimu ambapo huadhimishwa mwishoni mwa Mwezi Februari.

Amesema kuwa akiwa kama Kiongozi wa Serikali atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kuhakisha Serikali Inaweka Sera nzuri na madhubuti ambazo zitaweza kutoa kila aina ya msaada inayohitajika kwa watoto wenye magonjwa Adimu ikiwemo kushinikiza watoto kupata Oksijeni bure.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Taasisi ya Ali Kimara,Bi.Sharifa Mbarak amesema moja ya changamoto ambazo familia nyingi zenye watoto wenye magonjwa adimu ni gharama kubwa za matibabu hivyo ili kuweza kupunguza makali hayo wanaiomba serikali kuangia namna ya kuweza kutoa bure kwa mitungi hiyo ya gesi kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao kupumua.

Amesema anatambua kuwa kila mtoto anayo haki ya kupata elimu, kwa kulitambua hilo anawaomba wazazi wenye watoto wenye magonjwa adimu wahakikishe wanapata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine.

“Elimu ndio ufunguo wa maisha kwa kulitambua hilo mimi na muwe wangu tulipambana kuhakikisha Ali anasoma akiwa nyumbani kama walivyo watoto wengine,” Amesema.

Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya WatotoHospitali ya Agha Khan Dkt.Edward Kija amesema asilimia 6 yya watu duniani wanaugua magonjwa Adimu sawa na watu Laki Tatu nchini Tanzania tukitumia Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Mwenyekiti wa Taasisi ya Malcom Bi.Sarah Chande ameomba wadau wa afya nchini ikiwemo Serikali kuwepo na Elimu kwa jamii kuhusiana na magonjwa hayo ili jamii iweze kufahamu pamoja na kuepo kwa punguzo la umeme na msaada wa gesi ambayo watoto hao hutumia kwa muda wote.

Post a Comment

0 Comments