Mkurugenzi wa Menejimenti na Maarifa COSTECH Mhandisi Samson Mwela akifungua Mafunzo ya siku Mbili kwa waandishi wa Habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu ambayo yanafanyika kwa siku Mbili jijini Dar es salaam.
Mtafiti kutoka Taasisi ya TARI iliyopo Mikocheni Margareth Daudi akiwasilisha mada kuhusu ubunifu wa kuzalisha 'activated carbon'katika Mafunzo ya siku Mbili kwa waandishi wa Habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu ambayo yanafanyika kwa siku Mbili jijini Dar es salaam..
Mtaribu wa Mafunzo hayo Deusidedith Bagambe akitaja malengo ya Mafunzo ya siku Mbili kwa waandishi wa Habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu ambayo yanafanyika kwa siku Mbili jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanahabari Pamoja na watafiti ambao wameshiriki katika Mafunzo ya siku Mbili kwa waandishi wa Habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu ambayo yanafanyika kwa siku Mbili jijini Dar es salaam.
............................
NA MWANDISHI WETU
Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imewasisitiza wanahabari kuendelea kuwa mabalozi wa kutangaza na kuandika taarifa za Sayansi na utafiti Ili kuleta mabadiliko chanya kwa Taifa.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es alaam na Mkurugenzi wa Menejimenti na Maarifa COSTECH Mhandisi Samson Mwela wakati akifungua Mafunzo ya siku Mbili kwa waandishi wa Habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu sambamba na ziara ya kutembelea vituo vya utafiti vinavyopokea uwezeshani wa serikali kupitia COSTECH.
Mwela amesema malengo yao ni kuhamasisha na kuwajengea molari waandishi wa habari ili waweze kuandika taarifa za Sayansi,Teknolojia na ubunifu.
"Utafiti inafanyika Ili kubadilisha Maisha ya watanzania hivyo tukio hili linasaidia kuwaonyesha wanahabari mambo yanayofanyika katika tafiti mbalimbali"amesema Mwela
Aidha amewasihi wanahabari kuwa wataendelea kuyafanyia kazi Mafunzo ambayo wamepewa Ili kuweza kuonyesha fursa ya zilizopo Tanzania katika nyanja ya utafiti.
Kwa upande wake Mtaribu wa Mafunzo hayo Deusidedith Bagambe akitaja malengo ya Mafunzo hayo amesema kuwa ni kuwahamasishwa na kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa habari kufahamu namna ya kuandika taarifa za Masuala ya Sayansi na Teknolojia.
Amesema kuwa wameamua kuwapa Mafunzo wanahabari hao kutokana na kufanya kazi ambazo zinahusiana na Masuala ya Sayansi na Teknolojia na hivyo kuielimisha jamii.
"Tutaendela kushirikiaa na wanahabari Pamoja na watafiti kwani dhamira yetu ni kuhakikisha taarifa zetu zinaifikia Jamii kila wakati jambo litakalosaidia kuweza kunufaika nazo"amesema Bagambe
0 Comments