Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa akifungua semina kwa viongozi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga
Na Halima Khoya - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imetoa elimu ya Bima Maisha , huduma mbalimbali za kibenki pamoja na uwezeshwaji Kibiashara kwa viongozi wa VICOBA (wanawake na vijana) Manispaa ya Shinyanga ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Mafunzo hayo kwa viongozi wa VICOBA yamefanyika leo Jumatano Machi 15, 2023 katika ukumbi wa Empire hotel Mjini Shinyanga.
Akifungua mafunzo hayo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana amewataka wana kikundi hao kukata bima ya maisha kwa ajili ya kuwasaidia kipindi cha majanga kama vile kifo kwa mwanakikundi , mwenza wake , mtoto au kupata ulemavu wa kudumu kwa mwanachama mwenyewe akitolea mfano wa Fao la Amani ambalo mteja huchangia 4000/= kwa mwezi na pindi mwanakikundi akifarikidunia benki inatoa pole ya shilingi milioni 10, mwenza milioni 5 , mtoto milioni 3, akipata ulemavu wa kudumu shilingi milioni 10.
Pia amesema benki ya CRDB inatoa bima zingine kwa ajili ya kukinga majanga kama moto, kwenye biashara, nyumba, magari, pikipiki hivyo kuwasihi viongozi hao wa VICOBA kuwa mabalozi kwa wanachama wenzao na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Meneja Biashara wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy amewashauri wanakikundi hao kufungua akaunti ambazo hazina riba wala makato ambazo zitasaidia kuwainua kiuchumi wanavikundi na wananchi katika sekta mbalimbali.
Mwanahamisi amezitaja miongoni mwa akaunti zilizopo katika Benki ya CRDB ni pamoja na Junior Jumbo, Fixed Deposit, Malkia account, Dhahabu account , Fahari Kilimo, Hodari account, Nia Moja account na Islamic account ambazo zinatoa huduma bora na zenye kuaminika katika jamii.
Afisa Mahusiano Biashara za Bima Benki ya CRDB tawi la Shinyanga ,Jacob Elias amesema kuwa umuhimu wa bima kwa wanavikundi ni kupata mafao wanapopata changamoto yeyote kulingana na ukubwa wa bima aliyoikata ambapo kwenye bima kuna bima ya magari,nyumba na pikipiki sambamba na bima kwa wanakikundi inayosaidia kutatua tatizo na kutoa msaada wa haraka zaidi.
Kwa upande wake Mchambuzi wa Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Samson Ngwaltu, ametumia fursa hiyo kutambulisha rasmi Programu ya iMBEJU ambayo inalenga kutoa mafunzo, ushauri, na mitaji wezeshi kwa vijana na wanawake.
“Kwa vijana ambao ni wabunifu siyo lazima awe na akaunti ndiyo apewe mtaji wezeshi bali ni ubunifu wake ndiyo utamfanya afaidike na benki yetu, vijana ni lazima wapitie katika ofisi ya TEHAMA wilayani ili apewe cheti kitakachomuwezesha kupata huduma za kibenki lakini kwa wanawake wanaenda moja kwa moja benki na kueleza ubunifu wao”, amesema Ngwaltu.
Naye Meneja Mahusiano Kilimo Biashara, Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda amesema upatikanaji wa mikopo kwa wakulima hulingana na hali halisi ya maisha ya mwanakikundi ambapo dhamana yake ni mali zisizohamishika huku wanavikundi wakiahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopatiwa na watoa elimu benki ya CRDB ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa akifungua semina kwa viongozi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga
Mchambuzi wa Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Samson Ngwaltu akitoa elimu kwa viongozi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga
Mchambuzi wa Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Samson Ngwaltu akitoa elimu kwa viongozi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga
Meneja Mahusiano Kilimo Biashara, Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Meneja Mahusiano Kilimo Biashara, Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Meneja Mahusiano Biashara za Serikali Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Yohana Bunzali akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Meneja Mahusiano Biashara za Serikali Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Yohana Bunzali akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Meneja wa CRDB tawi la Shinyanga,Luther Mneney akizungumza kwenye Semina kwa viongzi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga.
Meneja wa CRDB tawi la Shinyanga,Luther Mneney akizungumza kwenye Semina kwa viongzi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Biashara wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Meneja Biashara wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy akizungumza kwenye semina ya utoaji elimu kwa viongozi wa VICOBA Shinyanga.
Viongozi wa VICOBA Manispaa ya Shinyanga wakiendelea na semina.

0 Comments