Ticker

6/recent/ticker-posts

WAWEKEZAJI WA VIWANDA TANGA WALIA NA KERO YA UMEME, RC AWATOA HOFU

Meneja wa kiwanda cha kuchakatia Mkonge cha Amboni Spinning Mill, Robert Semwaiko akimpa maelezo kuhusu kamba za katani zinavyochakatwa mpaka kufikia kufungwa.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Mamujee jijini Tanga Fatma Mamujee akisikiliza maelezo ya mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Omari Mgumba akikabidhiwa boksi la mafuta na Msimamizi wa kiwanda cha mafuta ya kujipaka cha Mamujee alipotembelea kiwandani hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Omari Mgumba wa tatu Toka kushoto mbele akiwa na viongozi wa ulinzi na usalama Mkoa katika kiwanda cha kutengeneza vocha jijini Tanga, kulia kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rashid Liemba.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Omari Mgumba akiongea na waandishi wa habari baada ya kukagua kiwanda cha Nillkant ambacho kinazalisha maligafi ya klinka pamoja na chokaa kilichopo Amboni jijini Tanga.


***********************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


TATIZO la kukatika kwa umeme mara kwa mara limekuwa kikwazo kikubwa katika uzalishaji maligafi kwenye viwanda vikubwa na vidogo kwa Mkoa wa Tanga.


Baadhi ya wawekezaji wa viwanda mbalimbali wametoa kero hiyo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alipofanya ziara katika viwanda hivyo ambapo wamesema mbali na kero hiyo zipo nyingine kwa baadhi ya viwanda ambazo husababisha uzalishaji kukosa tija.


Akiwa katika kiwanda cha Nillkant ambacho kinazalisha maligafi ya klinka pamoja na chokaa kilichopo Amboni jijini Tanga amesema pata kero ya umeme pamoja na barabara inayoingilia kiwandani hapo ambapo Mkurugenzi wa kiwanda Liemba alisema kwamba mara kwa mara ajali zinatokea kutokana na ubovu wa miundombinu hiyo.


Lakini pia katika kiwanda cha ambacho hutengeneza kadi za vitambulisho pamoja na vocha, Mkurugenzi wa viwanda hivyo Mohamed Liemba amesema kwakuwa wako kwenye mchakato wa kuanza uzalishaji kwa sasa hawana kero kubwa lakini aliiomba serikali kusaidia kutafuta masoko.


"Kiwanda hiki kwa sasa kipo katika mchakato wa kuanza kuzalisha, hapa tunazalisha kadi za benki mbalimbali na kadi za nida hivyo tunaiomba serikali itupe msaada wa kututafutia oda katika masoko, tukishapata tu tupo tayari kuanza uzalishaji" amebainisha" Liemba.


Naye Meneja wa kiwanda cha kuchakatia Mkonge cha Amboni Spinning Mill L.t.d Robert Semwaiko amesema serikali ina wajibu wa kutekeleza kero za wawekezaji na kuzitatua kabla hawajakata tamaa na kushindwa kufanya uzalishaji.


Semwaiko amebainisha kwamba pamoja na kero nyingine pia kuna ukakasi mkubwa katika suala la kamba za katani wanazotengeneza na zile za plastiki kutoka nje ambazo zimeonekana kufikisha biashara ya kamba zao.


"Tatizo jingine kubwa ni ujio wa hizi kamba za plastiki, kwa sababu mbali ya kupoteza ajira kwa kupunguza wafanya kazi lakini pia zanaharibu mazingira yetu ya ardhi" amesema Semwaiko.


Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha wanatembelea viwanda vyote vikubwa na vidogo mkoani humo ili kutimiza azma ya Rais Samia Sulluhu Hassan kuifanya Tanga kuwa ya viwanda kama ilivyokuwa awali.


"Kwahiyo nimekuja kuwasikiliza, kukagua shuhuli zenu zinaendeleaje na kusikiliza kero zenu ili tuzitatue kwa pamoja na Ustawi huu wa viwanda urudi katika nafasi yake, mkistawi ninyi na wengine wengi watakuwa kuwekeza, lakini mkiwa mnalialia hakuna mwekezaji atakayekuja kuwekeza katika Mkoa huu" amebainisha.


"Na ndio maana nikauliza kwanini viwanda vingi hapa vimekufa na vimegeuka magofu, lengo letu hapa siyo kumtafuta mchawi, ni kwamba tunataka kuvifufua na tuangalie tulikosea wapi ili tusirudie kosa lililofanyika huko nyuma"" amesema.


Amebainisha kero za kukatika kwa umeme, barabara ya kutoka mjini yanapoingilia kwenda kiwandani pamoja na upanuzi wa Bandari ya Tanga alisema uboreshaji utafanyika baada ya kukaa na kamati zake kujadili na kufikia muafaka.


"Suala la kukatika kwa umeme ni la nchi nzima na kama mnavyoona kuna mradi mkubwa ambao unatekelezwa kwa sasa, lakini kuhusu barabara ya kuingia kiwandani hapa tutalichukua na kwenda kukaa na viongozi wenzangu tuone hata kama hatukupata lami lakini tupate hata changarawe" amesema.


Kwa upande wa kiwanda cha mkonge Mgumba amesema kero zao ni kubwa na zenye mashiko kwani linapozungumziwa suala la Mkonge lina wigo mpana ambalo kama serikali ikae na kuziangalia kero zao na kuzitatua kwakuwa uwekezaji wa zao hilo ni mkubwa na unahitaji uangalizi wa kina.


"Unapozungunzia Mkonge ndiyo Tanga, asilimia 80 wananchi wanategemea kilimo hiki, na umuhimu wa kiwanda hiki ni mkubwa sana na kero yao ya kutozwa kodi kubwa kwenye mashamba ya mkonge yaliyopo mjini, ikumbukwe kwamba mashamba haya yalianzishwa kabla ya ukoloni mpaka sasa",


"Kwahiyo mabadiliko ya sheria ya ardhi iliyoanzishwa iliyakuta mashamba yale yako mjini, hivyo mashamba kutozwa sh elfu 5 na vijijini kulipa sh elfu 1 tumeona wana hoja ya msingi, itabidi sheria ile iangalie upya, tujue kama itaanzia pale ilipotungwa, kwamba litakapoanzishwa shamba jipya mjini ndiyo litozwe kodi hiyo" amebainisha.

Post a Comment

0 Comments