Ticker

6/recent/ticker-posts

VODACOM M-PESA KUSHIRIKIANA NA WAFANYBIASHARA KUWAZAWADIA WATEJA WANAOFANYA MALIPO YA KIDIJITALI MSIMU HUU WA WAPENDANAO.

Mkuu wa Idara ya Lipa kwa Simu, Vodacom Tanzania PLC Bw.Killian Kamota akizungumza na waaandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ iliyozinduliwa leo Februari 10,2023 na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Lipa kwa Simu, Vodacom Tanzania PLC Bw.Killian Kamota (katikati) akizungumza na waaandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ iliyozinduliwa leo Februari 10,2023 na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dar es Salaam Meneja wa Mr. Price Mlimani city, Bi.Anna Mwakitwile akizungumza na waaandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ iliyozinduliwa leo Februari 10,2023 na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dar es Salaam Meneja wa KFC Mlimani City B. Verynice akizungumza na waaandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ iliyozinduliwa leo Februari 10,2023 na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dar es Salaam Mmoja wa wateja katika duka la Mr. Price Mlimani City Jijini Dar es Salaam akilipia kwa simu kupitia Vodacom M-PESA baada ya kununua bidhaa kutoka Mr .Price na kupewa punguzo la asilimia 10% baada ya kufanya malipo kupitia lipa kwa simu katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ iliyozinduliwa leo Februari 10,2023 na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dar es Salaam

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc leo imezindua ‘Lipa Kwa Simu Valentine Campaign’ itakayowazawadia wateja wanapotumia simu zao za mkononi kufanya manunuzi kwenye maduka maalumu kama vile Mr. Price au kulipia huduma kwenye hoteli na migahawa mteja atarudishiwa asilimia 10% ya manunuzi ambayo ameyafanya.

Akizungumza leo Februari 10,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Lipa kwa Simu, Vodacom Tanzania PLC Bw.Killian Kamota, amesema kampeni hiyo mpya inayohamasisha malipo ya kidijitali pia ina lengo la kueneza upendo kwa wateja wanaotumia M-Pesa kufanya malipo ya kidijitali kwa kurudishiwa kiasi cha malipo yao papo hapo, kupata punguzo za bei na kupewa huduma za kimanunuzi zenye upekee.

“Huu ni msimu wa upendo na tunajua wateja wetu watakuwa kwenye shamrashamra, wakikununua zawadi na kufurahia kipindi hiki na wapendwa wao. Wakati wanafurahia usalama na urahisi wa kutumia huduma yetu ya Lipa kwa Simu kwa malipo katika maduka maalum ya rejareja na jumla, watapokea marejesho ya papo hapo ya 10% ya kiasi kilichotumiwa pamoja na ofa zingine za msimu huu wa wapendanao" alisema Mbeteni.

Amesema kupitia kampeni ya valentine ya Lipa kwa Simu, Vodacom na washirika wake watawazawadia wateja katika hoteli, migahawa na maduka ya rejareja yaliyochaguliwa kwa kuwarudishia kiasi cha pesa, punguzo maalum na huduma za maduka zitakazo wafanya wajisikie wakipekee.

Aidha amesema Vodacom M-Pesa ni huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi inayoongoza nchini Tanzania yenye lengo la kuifikisha nchi kwenye uchumi usiotegemea pesa taslimu kupitia bidhaa na huduma zake mbalimbali kama vile Lipa Kwa Simu, M-Pesa Visa, M-Pawa, M-Koba na nyinginezo nyingi kama sehemu ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali na kubadilisha maisha kupitia teknolojia.

"Ninawaomba wateja kuchukua fursa hii kueneza upendo na furaha wanapofanya malipo kupitia M-Pesa ili sio tu kufurahia punguzo na ofa hizi kubwa bali pia kufurahia usalama na urahisi wa malipo ya kidijitali katika mwezi huu wa Valentine" . Amesema Bw.Kamota

Akizungumza kwa niaba ya washirika wengine, Meneja wa Mr. Price Mlimani city, Bi.Anna Mwakitwile amesema wanayofuraha kushirikiana na Vodacom M-Pesa ili kuwapa wateja wetu uzoefu wa kipekee wa kufanya manunuzi na zawadi kwa ajili yao na wapendwa wao katika msimu huu wa wapendanao.

"Siku ya Valentine Day ukinunua bidhaa kwenye duka letu kuanzia shilingi elfu 50 na kuendelea utapata asilimia 10% ya manunuzi yako, pia duka letu linaupande wa nguo na upande wa home, upande wa home ni vitu vya nyumbani pia kutakuwa na punguzo". Amesema Bi.Anna Mwakititwile.

Post a Comment

0 Comments