Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAAMBULIA SARE MBELE YA AZAM FC



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeambulia sare kwenye mechi yake dhidi ya Azam Fc katika mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Azam Fc walifanikiwa kupata bao la mapema kabisa dakika ya 1 ya mchezo baada ya mpira kuanza.

Price Dube kwa mara nyingine tena ndio amefunga bao pekee la Azam na kuwafanya waongoze kwenye mchezo huo mpaka dakika ya 90 ya mchezo kabla ya Simba sc kusawazisha kupitia kwa Kibu Dennis.

Post a Comment

0 Comments