***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imeendelea kuuwasha moto kwenye ligi ya NBC hasa kwa kutoa dozi za uhakika kwa timu za ligi hiyo ambapo leo imefanikiwa kuichapa timu ya Singida Big Stars kwa mabao 3-1.
Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, tumeshuhudia mshambuliaji raia wa Congo Jean Baleke akiweka kambani tena kwa mara nyingine tokea alivyojiunga na miamba hiyoya msimbazi.
Haikuishia hapo tu, nyota wa timu hiyo Saidi Nitbazonkiza nae alifanikiwa kuingia kambani tena kwa kufunga bao la pili kwenye mchezo huo ambalo liliwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1 huku bao pekee la Singida Big Stars likifungwa na Bruno Gomez
Bao la tatu la Simba Sc lilifungwa na Osman Sakho akipokea krosi kutoka kwa Shomari Kapombe, bao ambalo liliwashua mashabiki wengi kwani linataka kufanana na lile ambalo alifunga kwenye michuano ya CAF mwaka jana.
0 Comments