Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akizungumza wakati wa Semina ya Kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akiongoza Semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa kamati yake iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Judith Kapinga akichangia mjadala wa nishati ya kupikia wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wabunge iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katka ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Stephen Byabato akitoa majumuisho ktk Semina ya Kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati.
***********
Serikali imeandaa mpango wa kutoa ruzuku ambayo kwa ajili ya kusambaza majiko na mitungi ya gesi yakupikia 100,000 katika maeneo ya vijijini katika mikoa 25 ya Tanzania Bara.
Mkurugenzi Mkuuwa REA, Mhandisi Hassan Saidy alisema hayo Katika Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati Jijini Dodoma.
“Pia tuna mpango wa kusambaza majiko banifu 200,000 yanayo tumia kuni na mkaa kidogo ilikupunguza uvunaji wa miti na gharama zake zitakuwa nafuu” alisema Mhandisi Saidy.
Mhandisi Saidy alisema kuwa utekelezaji wa Mpango huo utatumia utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wasambazaji wa bidhaa na teknolojia za nishati bora na salama ya kupikia pamoja na kuwajengea uwezo wasambazaji hao ili waweze kupunguza bei ya majiko hayo na kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi maeneo ya vijijini.
Akitoa majumuisho katika Semina hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Wakili Stephen Byabato alisema kuwa Serikali imeandaa mpango wa kutoa ruzuku kwa wasambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia na bidhaa nyingine za nishati bora ya kupikia kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa hizo katika maeneo ya vijijini.
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dustan Kitandula alipongeza Wizara ya Nishati kwa kubuni miradi ya kusambaza nishati safi na salama ya kupikia maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Judith Kapinga aliitaka Serikali kwa kushirikiana na wasambazaji wa Mitungi ya gesi ya kupikia kuweka utaratibu ambao utawezesha wanachi wengi wa vijijini kutumia gesi hiyo.
“Tuweke mkakati na wasambazaji wa gesi ili ifike vijijini na iwe rahisi kwa wananchi kupata bidhaa hiyo” alisisitiza.
Vile vile wajumbe wa Kamati hiyo wameishauri Serikali iandae mpango utakaowezesha kupunguza gharama za majiko na gesi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.
Akichangia katika Semina hiyo, Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu alipendekeza kuwe na punguzo la bei kwa mitungi ya gesi ya kupikia kwa wananchi wa vijijini.
“Serikali imetofautisha bei ya umeme maeneo ya mijini na vijijini na kwenye gesi napo wafanye hivyo hivyo ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kutumia gesi kwaajili ya kupikia” alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Msalala, Mhe. Idd Kassim Idd alihoji kuwa Serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa Mitungi ya gesi ya kupikia inapatikana maeneo ya vijijini.
“ Bei ya mitungi ya gesi ipojuu kulinganisha na vipato vya wa nanchi wengi wa vijijini” alisema.
0 Comments