Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI 7, IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Zambia hapa nchini Mhe. Mathew Jere mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Zambia hapa nchini Mhe. Mathew Jere mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Pamoja na masuala mengine wamezungumzia pia kuhusu Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA pamoja na Bomba la Mafuta la TAZAMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Sherif Abdelhamid Imam Ismail mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Sherif Abdelhamid Imam Ismail mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Katika mazungumzo yao walisisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano katika Sekta ya Elimu Ulinzi na Uwekezaji kwenye Kilimo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Michael Battle mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya Biashara, Uwekezaji na Kilimo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Brazil hapa nchini Mhe. Gustavo Martins Nogueira mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Katika mazungumzo yao walisisitiza masuala ya Afya ya Mama na mtoto, maradhi ya Seli Mundu (Sickle cell) pamoja na kuendelezwa kwa ushirikiano kwenye Sekta ya Kilimo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Askofu Mkuu Angelo Accattino mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Vatican hapa nchini Askofu Mkuu Angelo Accattino mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Katika Mazungumzo yao wamegusia kuhusu kushirikiana zaidi kwenye Afya, Elimu, Mazingira na Amani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino hapa nchini Mhe. Marie Charlotte G. Tang mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Ufilipino hapa nchini Mhe. Marie Charlotte G. Tang mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Wamezungumzia masuala ya Kilimo na Uvuvi ambayo nchi ya Ufilipino imepiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Romania hapa nchini Mhe. Dragos-Viorel -Radu Tigau mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Romania hapa nchini Mhe. Dragos-Viorel -Radu Tigau mara baada ya kupokea Hati yake ya utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023. Katika Mazungumzo yao wamesisitiza zaidi masuala ya Elimu na Teknolojia.

Post a Comment

0 Comments