Ticker

6/recent/ticker-posts

POLISI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI WA KATA KUPINGA UHALIFU.


Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Nchini limewataka Watendaji Kata pamoja na Askari Kata kushirikiana kwa pamoja kupinga na kukemea vitendo vya kihalifu hususani ukatili wa Kijinsia katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Jamii Nchini CP. Faustine Shilogile leo Februari 14, 2023 wakati akizungumza na Watendaji wa Kata pamoja na Wakaguzi wa Kata za Jiji la Arusha tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji hilo.

CP Shilogile amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusiana na madhara ya uhalifu hususani vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekua vikiongezeka katika jamii.

Sambamba na hilo pia ameongelea suala la utalii ambapo amebainisha kuwa viongozi hao wanaowajibu wa kuhakikisha watalii wanaofika katika jiji hilo wanakua salama wakati wote na kuwataka kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vitaimarisha usalama katika Jiji hilo.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bwana Elija Kondi wakati akiwasilisha mada amesema lengo la kikao hicho ni kujenga uelewa wa pamoja baina ya Jeshi la Polisi na Serikali za mitaa ili kufanikisha suala zima la ushirikishwaji wa jamii katika kufichua vitendo vya kihalifu.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha bwana Hargeney Chitukuro pamoja na kushukuru kwa elimu waliyoipata pia amesema uongozi wa Jiji hilo utahakikisha unaboresha mazingira ya kiutendaji baina ya Polisi kata na Watendaji wa kata ili dhana nzima ya Polisi jamii ilete matokeo chanya katika kata zote za jiji la Arusha.

Jeshi la Polisi Nchini kupitia Kamisheni ya Polisi jamii lipo katika ziara ya kuzunguka Nchi nzima kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja baina ya Jeshi la Polisi, Kamati za ulinzi na usalama Mikoa na Wilaya zote nchini pamoja serikali za mitaa kuhusu suala zima umuhimu wa kushirikisha jamii katika kufichua matukio ya uhalifu.

Post a Comment

0 Comments