MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiongoza Matembezi ya Kupinga Vita Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto, na kutimiza Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, matembezi hayo yaliyofanyika katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na kujumuika na Watoto wa Skuli mbalimbali katika matembezi hayo yaliyoazia Kendwa na kumalizikia katika viwanja vya mpira Nungwi.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation. Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiongoza Matembezi ya Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na Kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, akiwa na baadhi ya Watoto wakishiriki matembezi hayo yaliyoazia katika eneo la Kendwa na kumalizika katika viwanja vya mpira vya Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi Omary na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud .(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akishiriki katika mazoezi ya pamoja ya viungo baada ya kumaliza kwa Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, mazoezi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 19-2-2023, na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akijumuika na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Fujoni wakati wakiimba wimbo maalum wa kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa Watoto wakati wa hafla ya Matembezi ya Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, iliofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar.Mhe. Riziki Pembe.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli za Msingi za Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakiwa na mabongo yenye ujumbe wa “Udhalilishaji kwa Watoto haukubaliki” wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwahutubia katika viwanja vya mpira vya Nungwi, wakati wa Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation.(Picha na Ikulu)
0 Comments