Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Dar ea Salaam Khadija Ally Said amepata fursa ya kufanya mazugumzo na Kamishna wa Skauti Mkoa huo Amina Maulid na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu ushirikiano.
Mengine ni kujua mchango na utayari wa Chama cha skauti katika utoaji wa mafunzo, elimu na malezi ya watoto na vijana kwa ujumla na namna ambayo jumuiya ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Februari 20,2023 na Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ,katika mazungumzo hayo wamejadiliana kwa kina kuhusu kushirikiana na Chama cha Skauti Dar es Salaam kama wadau na kutoa mchango wa pamoja kwenye kulinda maadili ya watoto na vijana kwa ujumla.
Aidha kuelimisha kuhusu mmong'onyoko wa maadili na athari zake unaojitokeza kwenye jamii yetu kwa kasi kubwa sasa hivi na kwamba
Jumuiya ya wazazi Dar es salaam imeazimia kushirikiana na Skauti Dar es salaam kuwa na Klabu za Skauti katika kata zote 102 za Mkoa huo.
0 Comments