Ticker

6/recent/ticker-posts

MUSOMA: FEDHA ZA TASAF ZABADILISHA MAISHA YA JOSEPHINE BRUNO KWA MRADI WA KOKOTO



Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma Josephine Bruno akionesha nyumba yake haipo pichani ambayo iko karibu na mradiwake huo wa kokoto manispaa ya Musoma. 

Mkazi wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma mkoani Mara Bi. Josephine Bruno akiponda kokoto ambao huziua kwa watu mbalimbali wanaofanya ujenzi mradi ambao ameuanzisha baada ya kunufaika nafedha za mpango wa kunusuru kaya masikini kutoka TASAF ambapo sasa anawezakuenesha maisha yake vizuri tofauti na hapo awali. 


Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma Josephine Bruno akizunguma na Bi.Faraja Luhanjo kutoka TASAF wakati alipotembelea mradi wake wa kokoto mjini Musoma. 


Baadhi mawe ambayo wamekuwa wakiponda na ktengeneza kokoto kwa ajili ya kuuza. 


Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma Josephine Bruno aki akitoa baadhi ya taarifa zake kwa Bi. Faraja Luhanjo kutoka TASAF wakati alipotembelea mradi wake wa kokoto mjini Musomaanayeandika taarifa hizo ni Afisa Mtendaji wa katika moja ya mitaa ya Kata ya Mwisenge Bw Paul Masige Nyambarya. 

........................................................... 

Mkazi wa Manispaa ya Musoma ameipongeza TASAF kwa kuendelea kumsaidia kujinasua katika umaskini na kujimarisha kiuchumi katika utekelezaji wa mpango wake wa kunusuru kaya masikini nchini Tanzania. 

Akizungumza Februari 13 ,2023 Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma Bi. Josephine Bruno ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mpango wa kunusuru Kaya masikini chini ya TASAF ambaye ni miongoni mwa wanufaika waliokuwa wakihudumiwa katika mpango huo kwa muda wa miaka 8 amesema fedha hizo zimemsaidia sana kufanikisha shughuli zake kwa urahisi. 

Aidha amesema tangu ameingia TASAF amefanikisha malengo yake ya kuponda kokoto mwenyewe na kujipatia faida kupitia pia watu anaowaajiri kwa ajili ya kuponda kokoto ilikuuza lakini pia kuwasomesha watoto wake. 

"Nilikuwa sina mradi wowote lakini baada ya kupata fedha za TASAF nilianza kufuga kuku lakini baadae wakafa hivyo nikaona watanisumbua nikaanza kufuga bata huku nikiuza baadhi nakuingiza kwenye mradi huu wa mawe ambao ninaajiri mtu halafu namlipa," amesema Josephine Bruno 

Ameishukuru TASAF kwa kumuwezesha kujipatia mradi huo wa kuponda mawe kwani kwake umekuwa ni endelevu na mkombozi wa maisha yake ambapo unamsaidia katika maisha yake na familia yake. 

Ameongeza kuwa moja ya manufaa kutoka TASAF imemsaidia mtoto wake wa kiume kumsomeshwa VETA na kuchaguliwa katika kazi ya kuchomelea ambayo mbali ya kuongeza ujuzi wake lakini pia inampatia kipato japokuwa ni kidogo kwa sababu bado hajapata ajira. 

Amefafanua kuwa mtoto wake mwingine amemsomesha kwa kupitia pesa ya TASAF ambapo nilikuwa nikiingiza kwenye mradi na faida ambayo nilikuwa naipata ndo nikawa naipeleka chuo ilikumlipia ada mtoto wangu hivyo naishukuru TASAF sana’amesema Josephine 

Josephine ametumia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutolemaa na pesa ya TASAF ikiwemo kufanyia starehe badala yake waitumie katika maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ilikuwekeza na kiasi cha faida kinachopatikana wawasomeshe watoto. 

Hata hivyo Josephine licha ya kunufaika na TASAF yeye pamoja na wenzake wanaondoka kwenye mfumo wa huduma hiyo baada ya kuhitimu na uchumi wao Kuimarika Sasa wanaendelea na shughuli zao ndogondogo za kujiongezea kipato na kuendesha maisha Yao

Post a Comment

0 Comments