Ticker

6/recent/ticker-posts

MTUHUMIWA KESI YA WIZI MALI ZA MAREHEMU A AJALI AJINYONGA AKIWA RUMANDE.



Na Hamida Kamchalla, TANGA.


MMOJA wa watuhumiwa kati ya watuhumiwa nane wanaoshikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Tanga kwa wizi wa mali za marehemu amekutwa amejinyonga akiwa mahabusu.


Marehemu anahusishwa na kuiba mali za marehemu wa ajali iliyotokea usiku wa kuamkia February 3 mwaka huu iliyotokea wailayani korogwe iliyohusisha na kusababisha vifo vya watu 17 papo hapo na kujeruhi 12 ambao wengine watatu waliaga dunia wakiwa hospitalini.


Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati mkutano wa makabidhiano ya utoaji saini mikataba ya miradi 9 ya maji ya Wakala wa Maji Vijijini na usafi wa mazingira Mkoa wa Tanga (RUWASA mkoani humo.


Mgumba amesema katika msako uliofanyika watu 12 walikamatwa na baada ya uchunguzi watuhumiwa 8 kati yao walifikishwa mahakamani ambapo mpaka kufikia usiku wa februari 23 mmoja alikuwa amejinyonga.


"Niwape taarifa kwamba, hivi karibuni tulipata msiba wa ajali mbaya sana katika Mkoa wetu wa Tanga, lakini kulikuwa na jambo la aibu lililotokea kwa majeruhi na marehemu wale, watuhumiwa 12 tuliwakamata, na baada ya uchunguzi watuhumiwa nane tuliwafikisha katika vyombo vya sheria wapo mahakamani,


"Na kwa bahati mbaya sana mmoja wapo ambaye tulimkamata na nguo za marehemu zilizojaa damu, simu na mabegi yake, usiku wa leo amejinyonga, lakini tumebaki na watuhumiwa 7 ambao wanaendelea kushikiliwa na vyombo vya sheria" amebainisha

Post a Comment

0 Comments