Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar akizungumza katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde akiwa katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam. Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakiwa katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Mawaziri, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Viongozi wa Mashirika ya Maendeleo wakiwa katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" . Mkutano huo umefanyika leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wadau maendeleo nchini kuoanisha jitihada zao za maendeleo pamoja na jitihada za Serikali ili kuwa muunganiko wa nguvu katika vipaumbele vya Serikali na kuleta tija kwa wananchi ambao ni wanufaika wa mipango ya maendeleo.
Ameyasema hayo leo Februari 14,2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu "Kuongeza Kasi ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa" .
Amesema kulikuwa na malalamiko ya wenzetu ambao tunafanya nao biashara kuhusu utitiri wa kikodi hivyo ni sehemu ambayo sasa wameshaiangalia " Rais alivyoingia madarakani alishafuta zaidi ya tozo 114 kwahiyo tunauhakika wa hivyo utaendelea kuvutia ukiangalia kwenye sekta ya uzalishaji katika bunge lililopita mheshimiwa rais alifuta kodi na tozo mbalimbali zinazohusisha sekta hizo lengo likiwa ni kutengeneza sekta hizo zivutie". Amesema
Amesema wamesaini pia mikataba ya makubaliano na nchi mbalimbali kwaajili ya soko la bidhaa kwasababu vilivyokuwa vinavunja moyo kwenye sekta za uzalishaji ni utitiri wa kodi kwahiyo wamesaini makubaliano hayo kwenye masuala ya samaki na maparachichi kwa nchi mbalimbali na kusaidia pato la mtu mmoja mmoja kupanda.
Aidha Dkt. Mwigulu amesema lengo la serikali ili kikabiliana na mfumuko wa bei ikiwemo bei za vyakula ni kuongeza uzalishaji wa ndani ili kujitegemea na kuweza kuhimili majanga mbalimbali ikiwemo Uviki19, mizozo ya kivita pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amebainisha mikakati ya serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi ni uwepo wa sera ya uchumi wa buluu ambapo fursa zilizopo ni ujenzi wa bandari mpya pamoja na teknolojia katika ili kuendana na sera hiyo.
Hata hivyo nao wadau wa maendeleo wamesema dhumuni lao ni kuendelea kufanya kazi kwa akaribu mas serikali kwa kuzingatia sera na sheria zilizopo ili kuwa ma uchumi imara na ustawi wa maendeleo ya taifa.
0 Comments