Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AKABIDHI MAGARI NA PIKIPIKI KUTOKA TAMISEMI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi na Watumishi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023. (Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Angellah Kairuki na Mkuu wa Mkoa Manyara Makongoro Nyerere, Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo na Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo wakati akijaribu moja kati ya magari 54 yaliokabidhiwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) katika hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Afisa Mtendaji Kata ya Ng’ong’ona (Kulia) iliopo Dodoma moja kati ya Pikipiki 916 zilizotolewa kwa Watendaji Kata kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, katika hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watendaji Kata kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.

************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka Watendaji wa Kata na Viongozi wa Mikoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutumia vitendea kazi wanavyokabidhiwa na serikali katika kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasikiliza, kuwahudumia,kufuatilia miradi ya maendeleo na siyo kutumia kwa manufaa binafsi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.

Amewaagiza maafisa watendaji kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kwa kuhakikisha vikao na wananchi katika ngazi ya Vijiji na Mitaa vinafanyika kama inavyopaswa.

Makamu wa Rais amewaasa Maafisa Watendaji kata kuacha uzembe katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli nyingine za kijamii.

Amesema utoaji wa vitendea kazi hivyo pamoja na mambo mengine unalenga kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo wanayosimamia.

Pia amesema ni muhimu kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwa kutoa hamasa kwa wananchi ili wawe mstari wa mbele katika shughuli za uhifadhi ikiwemo kupanda miti na usafi wa mazingira ili kuwepo na maendeleo endelevu.

Pia Makamu wa Rais amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha fedha kiasi cha Shilingi laki moja inayopaswa kutolewa kwa Maafisa Watendaji wa Kata kama posho ya madaraka inatolewa kwa wakati na kupewa kipaumbele kabla hazijalipwa posho za vikao vingine vya Halmashauri.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha mfumo na utendaji wa Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia misingi ya Kikatiba na Kisheria iliyopo kwa kutambua kwamba, mfumo wa Serikali za Mitaa, ndio njia pekee ya kusogeza huduma karibu na wananchi lakini pia kuwashirikisha wananchi katika kuamua, kupanga na kuchagua vipaumbele vya maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewataka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuyatimiza vema majukumu yao hususani ya kusimamia shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.

Amewasisitiza Mameneja wa Mikoa na Wilaya waliokabidhiwa magari hayo kutumia katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao na si vinginevyo pamoja na kuyatunza na kuyafanyia ukaguzi na matengenezo ndani ya muda ili yaweze kudumu.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Angellah Kairuki amesema Wizara hiyo itaendelea kuimarisha ngazi za msingi ikiwemo kata kwa kutambua ndiyo kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi katika utoaji huduma.

Ameongeza kwamba mgao wa fedha zinazopatikana utaendelea kuelekezwa katika makundi hayo muhimu zaidi kuwawezesha katika kuratibu na kufuatilia shughuli za maendeleo katika maeneo ya vijiji, mitaa na vitongoji

Aidha Waziri Kairuki amesema lengo la vitendea kazi hivyo ni kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi, kurahisisha usafiri pamoja na kuimarisha mapato.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Kairuki amesema TAMISEMI inapanga kutumia biashara ya kaboni kama hatua ya kulinda mazingira pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Serikali inaendelea kulipa na kupandisha madaraja watumishi umma hapa nchini ambapo tayari kibali cha kupanda madaraja kwa watumishi 26491 ambao walisimama kwa muda mrefu kimetolewa.

Mhagama ameongeza kwamba serikali inatarajia kuongeza wahandisi pamoja na wakadiriaji majengo katika halmashauri ili kukabiliana na tatizo la ujenzi wa miundombinu chini ya kiwango.

Aidha amesema Serikali inathamini na itahakikisha kunakuwepo na rasimimali watu ya uhakika ambayo ndiyo chachu ya ujenzi wa uchumi.

Awali akihutubia hadhara hiyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo ametoa wito kwa serikali kufanya mapitio ili kutambua upande wenye tija katika ukusanyaji mapato hususani kodi ya majengo kati ya Serikali kuu na Tamisemi ili kupewa jukumu la ukusanyaji na kupata matokeo makubwa zaidi.

Chongolo amesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa baada ya kuanzishwa kwa TARURA kwani Halmashauri zimeondokana na mgawanyo usio sawa mapato kulingana na mahitaji katika ujenzi wa miundombinu na sasa vipaumbele vinawekwa sehemu zenye changamoto zaidi.

Aidha ameiomba serikali kuendelea kuongeza bajeti ya TARURA ili iweze kufungua zaidi miundombinu maeneo mengi zaidi yenye fursa na uzalishaji hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments