Ticker

6/recent/ticker-posts

MADAKTARI BINGWA 12 KUTOKA BENJAMINI MKAPA DODOMA, KUTIBU WAGONJWA ZAIDI YA 200 MKOANI TANGA


Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Japhet Simeo
Mkurugenzi Msaidizi wa hospitali ya Kanda ya rufani ya Benjamin Mkapa Dodoma.


**************************


Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WAGONJWA zaidi ya 200 katika Mkoa wa Tanga wenye magonjwa yanayohitajika kuonwa na madaftari bingwa wanatarajiwa kupatiwa huduma mbalimbali na wataalamu hao kutoka hospitali ya Kanda ya rufani ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma.


Zoezi hilo limeanza kufanyika leo, februari 27 litaendelea hadi machi 3 mwaka huu litafanyika katika hospitali ya rufani ya Bombo huku likishirikisha madaftari bingwa 12 wa vitengo mbalimbali.


Akitoa taarifa ya ujio wa madaftari hao, Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Japhet Simeo amesema jumla ya wataalamu 12 na 9 kati yao ni mabingwa wa magonjwa katika vitengo mbalimbali na wamekuwa kutoa huduma kama sehemu ya mkoba zinazopaswa kutolea katika kanda na Taifa kwenya meno ya Mikoa.


"Kwahiyo tunatarajia kupata wananchi wenye matatizo mbalimbali na kuanzia leo mpaka kufikia mwezi machi 2023 wanatazamia kuona wagonjwa zaidi ya 200, ni wale wenye sifa za kuonwa na madaftari bingwa" amesema.


Dr. Simeo amebainisha kwamba kwa kipindi kirefu sana haikuwa rahisi kuwaoma madaftari bingwa hasa kutoka kwenye taasisi kwa sababu hawakuwepo hivyo serikali ilichukua jukumu la kuwasomesha wataalamu wake na sasa imeona ni vema kuwatoa kwenda kusaidia maeneo mengine.


Aidha amesema, "sasa kwa hospitali yetu ya rufani ya Bombo kwa Mkoa wa Tanga tunaomba madaftari wetu watakavyo kwenda kunufaika kwa ujio wa wataalamu hawa, kwa kupata taaluma ambazo zitakuwa zikitumiwa na mabingwa wakati wa utoaji tiba".


Ameongeza kuwa kwa sasa serikali iko katika kuwakinga na kuwatibu wananchi wake ambao wako katika mazingira hatarishi, kwani zamani tiba za madaftari bingwa hazikuwepo nchini na ilipelekea wagonjwa kufuata huduma nje ya nchi lakini kwa sasa yale matatizo bobezi yote yanatibiwa ndani ya nchi.


"Nitoe wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga wale wanaopaswa kuonwa na madaktari bingwa kuweza kujitokeza kupata huduma ambayo imesogezwa karibu, mgonjwa atachangia kiasi kidogo cha fedha tofauti na ambavyo angekwenda kutibiwa Benjamin Mkapa" amesema.


Naye Mkurugenzi Msaidizi wa hospitali ya kanda ya rufani ya Benjamin Mkapa Dodoma, Henry Humba amefafanua kwamba lengo kubwa la ujio wao mkoani hapa ni kuwaona wagonjwa ambao wanaopaswa lakini pia kutoa uzoefu kwa madaktari walioko katika hospitali ya rufani ya Bombo.


"Katika kipindi hiki tutakacho kuwepo hapa madaktari wetu wa Mkoa wa Tanga watapata kujifunza na vitu vingine kutokana na uwekezaji unavyoendelea kwahiyo huu ni muda ambao tutakwenda kubadilisha uzoefu wa kielimu tulionao na wenzetu" amesema.


Dr. Humba ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha upasuaji wa ubongo, mifupa ya fahamu, mifupa na uti wa mgongo, amesema huduma za tiba zitakazotolewa kuwa ni upasuaji wa mishipa ya fahamu, mifupa, mfumo wa haja ndogo, magonjwa ya ndani, figo, moyo kwa rika zote, magonjwa ya watoto, macho, kunywa na meno pamoja na uzazi kwa wakina mama.


"Hizi ni huduma ambazo miaka ya nyuma iliyopita zilikuwa zinaweza kupatikana nje ya nchi au katika hospitali moja tu hapa nchini, hivi mjue huduma hizi zinapatikana hadi kwenye hospitali za kanda za rufani, huu ni uwekezaji mkubwa upiofanywa na serikali" amesema.


Hata hivyo ameeleza kwamba katika hospitali ya rufani ya Benjamin Mkapa zipo huduma nyingine zimeanzishwa na serikali kama vile maabara maalumu ya uchunguzi na upasuaji wa moyo ambayo hapo nyuma ilikuwa katika hospitali moja tu ya Taifa ya Muhimbili.


"Lakini pia kuna huduma mpya ya upandikizaji wa uroto, na uwekezaji mkubwa uliofanyika ni kuwepo kwa huduma ya magonjwa ya saratani, kama inavyojulikana kwamba wagonjwa wa saratani wanatibiwa hospitali ya Ocean Road, lakini sasa serikali imewekeza na inapatikana Benjamin Mkapa" ameongeza.

Post a Comment

0 Comments