Ticker

6/recent/ticker-posts

KATAMBI ASISITIZA UMUHIMU WA USHIRIKIANO NA MASHAURIANO KWA VYAMA VYA WAFANYAKAZI


Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi ,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama hicho kilichofanyika jijini Dodoma.




Rais wa Chama cha Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya,,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.



Sehemu ya Viongozi wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),Dkt. Paul Loisulie,akiapishwa kuwa Kiongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),Dkt. Paul Loisulie,aakisaini nyaraka mara baada ya kuapishwa kuwa Kiongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.


Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),wakiapishwa kuwa Viongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.


Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia uapisho wa viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.

................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali imekuwa ikishauriana na kushirikiana na vyama vya wafanyakazi hali inayosaidia kutatua changamoto zao kwa njia rafiki.

Akizungumza Februari 3, mwaka huu katika hafla ya kuapishwa viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) jijini Dodoma, Mhe. Katambi amesema vyama hivyo vimepiga hatua kubwa kwa kujadiliana na serikali kidiplomasia katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Amebainisha kuwa kutokana na ushirikiano na mashauriano hayo, serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa shughulikia hoja zao kwa wakati ikiwamo suala la nyongeza ya mshahara.

“Mambo yaliyofanywa na Rais kwenu yapo mengi yakupongezwa kuna suala la nyongeza ya mishahara kwa asilimia 23 kwa watumishi wa umma na sekta binafsi tumekuja pia tumeweka kima cha chini cha mshahara ambacho tayari kimetangazwa,”amesema.
Aidha, amepongeza chama hicho ni chachu ya maendeleo na amani ndani ya taasisi za elimu ya juu nchini.
Naye, Mwenyekiti wa THTU taifa, Dkt.Paul Loisulie, amemshukuru Rais Samia kwa usikivu na utendaji wake na kuahidi kuwa chama hicho kitaendelea kuunga mkono jitihada zake za kuboresho maisha ya watanzania.

Post a Comment

0 Comments