****************
Na Magrethy Katengu
KAMPUNI ya Vijana Real Estate inayojihusisha na uuzaji wa viwanja imekuja na suluhisho la uuzaji viwanja vilivyopimwa kabisa kwa gharama nafuu katika Mradi uliopo Kiromo-Bagamoyo ili kusaidia watu wenye kipato cha juu kati na chini wote ardhi .
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Azaidu Mohamedi wakati wakimpatia Ubalozi Mtangazaji Maarufu wa Maulid Kitenge wa kutangaza Viwanja vilivyopimwa na kupewa hati miliki vilivyopo Mradi wa Kiromo-Bagamoyo lengo ni kila Mwananchi popote alipo anayetamani kumiliki eneo apate ujumbe huo .
"Viwanja hivi vimeshapimwa na kila anayehitaji atalipia kidogokidogo kwa kuandikishiana akimaliza atakabidhiwa hati miliki yake ambayo inatambulika na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Watu ni uhakika Watanzania wekezeni katika ardhi kwani kila siku inapanda thamani karibuni tuwahudumie hatubagui "amesema Mkurugenzi
Naye Meneja Masoko wa Vijana Real Estate Flora Mlowola amesema wanajiamini uuzaji wa viwanja kwani viwanja vyao viko kilometa nane kutoka Bandari ya Bagamoyo Kilometa nne kutoka Barabarani vimeshapimwa ni halali kabisa na Maulid Kitenge ambaye ni Balozi wetu wa Vijana Real Estate kabla ya kusainiana Mkataba alikwenda kukagua ,” amesema Mlowola.
Kwa upande wake Balozi Maulidi Kitenge amesema “Rasmi mimi nakwenda kuvivaa viatu vya Ubalozi wa Vijana Real Estate, niwauzaji wakubwa wa viwanja wana mradi mkubwa huko Kiromo-Bagamoyo,” amesema Kitenge na kuongeza,
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia viwanja hivyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na uwekezaji kwani mji wa Bagamoyo unakwenda kuchangamka kutokana na Bandari hiyo ya kisasa inayotarajiwa kujengwa.
0 Comments