Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir pamoja na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche wakikabidhi sare na vifaa vya shule kwa wanafunzi wanufaika wa mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akitazama baadhi ya taulo za kike ambazo zimetengenezwa na wanafunzi wa klabu ya Champion ambayo imenufaika na mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada katika hafla ya kuwakabidhi sare na vifaa vya shule kwa wanufaika hao leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir, Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage, Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche pamoja na wadau wengine wa elimu wakikagua vyoo ambavyo vimejengwa kupitia mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada katika hafla ya kuwakabidhi sare na vifaa vya shule kwa wanufaika hao leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada. Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche akisoma hotuba yake katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada. Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Bi.Mwantum Mgonja akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Bi.Mwantum Mgonja akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa sare na vifaa vya shule kwa shule za sekondari wilayani Mkuranga ambazo zipo katika mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.Zoezi hilo limefanyika leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir, Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage, Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche pamoja na wadau wengine wa elimu wakipata picha ya pamoja na wanafunzi walionufaika na mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada katika hafla ya kuwakabidhi sare na vifaa vya shule wanufaika hao leo Februari 16,2023 Mkuranga mkoani Pwani.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, MKURANGA PWANI
Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya elimu nchini, Haki Elimu limetoa msaada wa sare na vifaa vya shule vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 60 kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 280 wanaotoka katika familia duni ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao ya sekondari bila vikwazo.
Msaada huo ni moja ya matokeo ya mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.
Akizungumza leo Februari 16,023 Mkuranga mkoani Pwani, Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage amesema Mradi huu wa miaka mitatu unafadhiliwa na serikali ya Kanada na unatekelezwa katika jumla ya shule 67 (34 Msingi na 33 Sekondari) katika Wilaya 12 za Tanzania bara ambazo ni pamoja na Masasi, Kilwa, Mkuranga, Tunduru, Arusha, Babati, Bariadi, Tabora, Ukerewe, Serengeti, Geita na Sumbawanga.
Amesema lengo kuu la mradi huu ni kupunguza mdondoko wa wasichana kwa kuhakikisha kuwa wasichana wanabaki shuleni na wanahitimu masomo yao katika mazingira ambayo ni rafiki na salama.
"Kwa kushirikiana na watalaamu mbalimbali katika ngazi ya Wilaya, mradi huu umewezesha utolewaji wa mafunzo ya kijinsia na ulinzi wa mtoto, utengenezaji wa sodo, uanzishaji wa madawati ya kuzuia ukatili shuleni na ugawaji wa vyerehani kwa ajili ya elimu ya ufundi na ushonaji wa sodo vyenye thamani ya shilingi milioni 57". Amesema Dkt. Kalage.
Aidha amesema kazi kubwa iliyofanyika kupitia mradi huu ni pamoja na kuboresha miundominu ya shule yenye thamani ya takribani shilingi milioni 330 kwa kujenga vyoo vyenye vyumba maalumu vya kujisitiri kwa ajili ya wasichana, ujenzi wa hosteli kwa wasichana na ujenzi wa visima vya maji shuleni.
Amesema zoezi la kutoa msaada wa sare na vifaa vya shule limefanyika kwa miaka miwili mfululizo ambapo mpaka sasa jumla ya wasichana 544 wamenufaika na msaada huo.
"Kwa kuwa wasichana hawa wanatoka maeneo tofauti na kwa kuzingatia sababu mbalimbali, HakiElimu imeamua kufanya hafla fupi ya kuzindua zoezi la ugawaji wa sare na vifaa vya shule kitaifa katika shule ya sekondari Dundani iliyopo Wilaya ya Mkuranga ambayo ni shule mojawapo ya mradi". Amesema
Nae Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada Bi.Helen Fytche amesema katika suala la elimu, Canada inaamini katika kutoa fursa sawa na kupata elimu bora kwa wasichana kama njia bora ya kuondosha vikwazo kwa wanawake na wasichana kijamii, kiuchumi na kisiasa kwani itaboresha fursa za kupata na ushiriki wao wa kisiasa na kiuchumi katika maisha nchini.
Amesema mabinti wa Kitanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kupata elimu salama, yenye ubora na kuzingatia jinsia. Mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia, kazi za nyumbani na ukosefu wa bidhaa na mazingira bora ya kujistiri wakati wa hedhi mashuleni ni changamoto katika maudhurio mashuleni.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir ametoa wito kwa mashirika ya siyoyakiserikali na wadau wa Maendeleo kushirikiana na Serikali kuhakikisha mtoto wa kiume analindwa dhidi ya vitendo vya ukatili sawa na mtoto wa kike.
Mhe.Khadija pia ameishukuru Haki Elimu kuchagua Wilaya ya Mkuranga kuwa miongoni mwa Wilaya 12 zinazonufaika na Mradi wa kupunguza mdondoko na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike (Girls Retention and Transition Initiative) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.
“Wakati tunaendelea kuangalia namna ya kuwanusuru watoto wakike dhidi ya ukatili pia tutambue watoto wetu wa kiume hawapo salama sana kwenye janga hili la ukatili kwani kumekuwa na matukio ya ulawiti kwa watoto hawa”. Amesema
0 Comments