Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi ambaye aliambatana na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
***************
Bujumbura (Burundi) na Dodoma (Tanzania), 10 February 2023
Wakati hali ya Burundi inaendelea kuimarika, KamishnaMkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi, Filippo Grandi, amesisitiza dhamira ya UNHCR ya kusaidia wakimbizi kurejea salama kutoka katika nchiwalizopewa hifadhi.
Tangu mwaka 2017, zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Burundi wamesaidiwa na UNHCR kurejea nchini kwao kwa hiarikutoka nchi jirani ikiwemo Tanzania.
Akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Burundi, Grandiamemshukuru Rais Evariste Ndayishimiye kwa juhudi za kuleta utulivu nchini Burundi.
“Tunaishi katika ulimwengu wenye fursa chache tu za kuwezakusaidia kutafuta suluhisho la kudumu kwa wale wanaolazimika kuyakimbia makazi yao.
Mara nyingi, migogoro hudumu kwa muda mrefu lakini ninafarijika kuonawakimbizi wa Burundi wanafanya uamuzi wa kurejeanyumbani baada ya miaka mingi uhamishoni. Sote tunapaswakufanya kazi ili kuhakikisha wanapata suluhisho la kudumu,” alisema Grandi.
"Juhudi za Serikali ya Burundi na wadaukatika kusaidia wakimbizi wa Burundi wanaorejea nyumbanizinatia moyo sana."
Grandi ametembelea eneo la Rugombo na kuonana na baadhiya wakimbizi ambao wamerejea nyumbani hivi karibuni na kushuhudia misaada inayotolewa na UNHCR na wadau ilikuwawezesha kujenga upya maisha yao.
Misaadainajumuisha usafiri, chakula, fedha taslimu, na vifaa vya nyumbani kwa wakimbizi wanaorejea Burundi.
Kwa kuzingatia ukubwa wa mahitaji, UNHCR imeamua kuboreshana kuimarisha misaada kwa wanaorejea.
“Hata hivyo, tunahitaji wadau wa maendeleo kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma, na shughuli za kijamiikwa wakimbizi wanaorejea. Hawa ni raia wa Burundi na wanahitaji kujumuishwa katika mipango ya maendeleo” Grandi aliongeza.
Burundi pia inahifadhi wakimbizi 80,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Grandi ametembelea kituocha wakimbizi cha Cishemere kilichopo Kaskazini Magharibimwa nchi na katika eneo linalopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kukutana na wakimbizi wanaokimbia machafuko na ukatili Mashariki mwa DRC.
Grandi amewasili mkoani Dodoma leo akitokea Burundi na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa, ni hatua za mafanikiozinazoendelea kutekelezwa katika kuboresha mazingira na mahitaji nchini Burundi kwa wale wanaoendelea kurejea.
Grandi pia ameshukuru utamaduni wa muda mrefu wa Tanzania wa kukaribisha wakimbizi na juhudi zinazoendeleaza kuwahudumia wale wanaokimbia migogoro na mateso.
Kwa takwimu, Tanzania inahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi duniani. Takribani wakimbizi na waomba hifadhi248,000 wengi wao kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaishi Tanzania.
"Shirika litaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali, Mashirika, na wafadhili, pamoja na wadau wa maendeleo, ilikuhifadhi na kutafuta suluhisho kwa wale wanaolazimikakuyakimbia makazi yao.” alisema Grandi.
Katika muktadha huo, UNHCR inapokea kwa furaha tangazola Umoja wa Ulaya la kutoa ufadhili wa Euro milioni 40 katika miaka ijayo kwa washirika wanaosaidia kuboreshamazingira ya urejeaji nchini Burundi.
Ufadhili huoutawanufaisha wakimbizi wa Burundi katika ukanda huu, pamoja na wale waliorejea nyumbani, kwa kuhakikishawanapata usaidizi wanaohitaji ili kuishi kwa usalama na heshima.
Ufadhili huo utajumuisha ulinzi na uthabiti, msaadawa kisheria, masuala ya ukatili wa kijinsia, ujuzi wa kusomana kuandika na shughuli za kilimo
0 Comments