Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia (EBARR) Dkt. Makuru Nyalobi akitoa ufafanuzi wa Ujumbe wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) ukiongozwa na Mratibu wa Kanda ya Afrika, Dkt. Ibrahima Sow wakati wa ziara ya kutembelea Mradi wa EBARR unaotekelezwa katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Jumatano (Februari 15, 2023).
Ujumbe wa GEF ukiongozwa na Mratibu wa Kanda ya Afrika, Dkt. Ibrahima Sow (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea mradi wa maji wa safi na salama unaoratibu na Mradi wa EBARR ulio chini ya usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Kijiji cha Kiegea Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Jumatano (Februari 15, 2023).
Ujumbe wa Ujumbe wa Mfuko wa GEF mtambo wa uzalishaji wa mafuta ya alizeti zinazotumika kwa na mashudu ya vyakula vya mifugo wakati wa ziara ya ujumbe huo kukagua Mradi wa EBARR unaotekelezwa na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ziara ya ujumbe huo leo Jumatano (Februari 15, 2023) Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Afisa Mazingira Mwandamizi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) Filippo Berarch akitazama mbegu za alizeti zinazotumika kwa ajili ya kutengeneza mafuta na mashudu ya vyakula vya mifugo wakati wa ziara ya ujumbe huo kukagua Mradi wa EBARR unaotekelezwa na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ziara ya ujumbe huo leo Jumatano (Februari 15, 2023) Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
********************
Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) umesema umeridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia MIfumo Ikolojia (EBARR) unaotekelezwa katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Hayo yamesemwa leo Jumatano (Februari 15, 2022) na ujumbe wa Mfuko huo ukiongozwa na Mratibu wa GEF Kanda ya Afrika, Dkt. Ibrahima Sow wakati wa ziara ya kutembelea Mradi huo katika Vijiji vinne vya Wilaya hiyo.
Dkt. Sow amesema GEF imedhirisha na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa visima virefu vinne, malambo mawili, majosho mawili, vitalu nyumba vitatu na mashine ya kukamulia alizeti ambapo miradi hiyo imeweza kuwa chanzo mbadala cha kuongeza kipato kwa wananchi.
“Miradi hii ina faida kubwa kwa wananchi wa Mpwapwa, natoa rai kwa jamii kuweza kuitunza na kuwasaidia kwa ajili ya kuleta manufaa ya sasa na kwa kizazi kijacho” amesema Dkt. Sow ambaye aliambatana na ujumbe kutoka Sekretarieti ya GEF
Sow amesema GEF itaendelea kufadhili miradi ya mazingira inayozunguka jamii ili kuongeza kasi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika maeneo ya vijijini sambamba kuhakikisha jamii inajishughulisha na kilimo rafiki kwa mazingira na kutolea mfano kilimo cha mbogamboga.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa EBBAR Kitaifa, Dkt. Makuru Nyalobi amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kusimamia vyema miradi hiyo ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ambayo inatarajia kuwanufaika wananchi wa vijiji vya Nghambi, Mbugani, Kiegea na Kazania.
Ameongeza kuwa Mradi huo pia unatekelezwa katika Wilaya nyingine nne ambazo ni Kaskazini ‘A’ Unguja (Zanzibar), Simanjiro (Manyara), Mvomero (Morogoro) na Kishapu (Shinyanga) na kueleza kuwa miradi hiyo imetekelezwa kwa kutumia mifumo ikolojia ambapo mipango ya matumizi ya ardhi imeandaliwa.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbugani, Aziza Mwinyimbweni amesema Serikali ya Kijiji hicho imejipanga katika kuhakikisha kuwa mradi huo unafikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji safi na salama.
Ujumbe wa GEF ulikuwa Jijini Dodoma tarehe 13 hadi 14 Februari, 2023 na kuendesha warsha kwa wadau na wataalamu wa mazingira kutoka Serikali Kuu, TAMISEMI, Wakala, Idara na Wakala za Umma na sekta binafsi kwa ajili ya kuibua vipaumbele vya miradi ya mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.
0 Comments