Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.
KATIBU Mkuu TUGHE Taifa Mhandisi Amani Msuya akiwasilisha salamu za TUGHE Taifa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TUGHE ,Tawi la EWURA Mhandisi Victor Labaa akitoa neno la shukrani wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.
Wajumbe wa Baraza wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.
...................................
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa utendaji wenye ufanisi.
Mhe. Makilagi, ametoa pongezi hizo wakati akifungua kikao cha tano cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Adam Malima, leo tarehe 8. 02.2023, jijini Mwanza.
“Ninaipongeza EWURA, kwa kazi kubwa ya udhibiti ambayo mmeendelea kuifanya, tumeona hasa kwenye bei za mafuta, kupunguza uchakachuaji, jinsi mnavyosimamia uagizaji mafuta kwa pamoja na mnavyopanga bei za maji,tunawashukuru sana kwa kuikomboa jamii, mmepunguza changamoto nyingi” alisema Mhe. Makilagi.
Mha. Poline Msuya, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile katika kikao hicho, amesema Baraza la Wafanyakazi ni nyenzo muhimu katika utendaji wa taasisi, kwani ni njia mujarab ya ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uamuzi wa masuala yanayowahusu kwenye utendaji wao wa kila siku.
Kwa upande wake, Katibu wa TUGHE Taifa, Mha. Amani Msuya, ametumia fursa hiyo kuipongeza EWURA kwa kuendelea kujali maslahi ya wafanyakazi wake na kusisistiza kwamba, upimaji utendaji wa wafanyakazi unapaswa kuwa wa wazi na usawa ili kuondoa malalamiko mahali pa kazi.
Aidha, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la EWURA, Mha. Victor Labaa, amesema Baraza litaendelea kushirikiana na menejimenti katika kuimarisha ufanisi wa utendaji kwa mustakabali wa EWURA na Taifa ujumla.
0 Comments