Meneja wa benki ya CRDB tawi la Bunda mkoani mara , Bw. Marwa Solomon akizunguma na waandishi wa habari mjni Bunda alipozungumzia Programu ya malipo ya Mpango wa kunusuru kaya za Walengwa TASAF kwa njia ya kielektroniki (E. Payments).
Bw. Fredson Samwel ambaye ni Afisa wa NIDA wilaya ya Bunda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu namna wanavyohakikisha wanarekebisha majina ya walengwa wa TASAF katika vitambulisho vya NIDA ili kuendana sawa na majina wanayojiandikisha TASAF.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bunda Bi, Jackline Maili akielezea mkakati wa halmashauri hiyo kuhamasisha walengwa kujisajili ili kulipwa fedha za TASAF kwa njia wa Mtandao E. Payments.
.....................................................
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Bunda mkoani mara , Bw. Marwa Solomon amesema benki hiyo itashirikiana vyema na serikali kuhakikisha fedha zote za wanufaika wa mfuko wa TASAF zinalipwa na benki hiyo kupitia programu maalum ya kuwalipa wanufaika hao Kwa njia ya kielekroniki (E. Payments)
Meneja huyo ameyasema hayo wakati alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu ushirikiano wa benki hiyo na TASAF wilaya ya Bunda kupitia mfuko wa kunusuru kaya za walengwa, ambapo kufikia robo ya mwaka huu wanatarajia kuwaingiza wanufaika wa mfumo huo katika mfumo wa malipo kupitia vitambulisho vyao vya Taifa au namba za NIDA.
Bw. Marwa amesema kuwa kupitia programu hiyo sasa benki hiyo itatoa fomu maalum kwa wanachama hao wa TASAF na Kisha kuwafungulia akaunti na baadaye kuingizwa kwenye mfumo utakaowawezesha kupokea fedha zao kutoka katika mfuko huo bila malipo yoyote.
Amesema kupitia programu hiyo sasa itasaidia kuwatambua wahusika kamili wanaostahili kupokea fedha hizo kutokana na mfanano wa majina yao katika vitambisho vyao na akaunti zao za benki watakazofunguliwa ili kupokea fedha kama serikali ilivyoagiza kuwa malipo ya serikali sasa yafanyike kwa njia za kielektroniki (E.Payments)
Naye Bw. Fredson Samwel ambaye ni Afisa wa NIDA wilaya ya Bunda amesema kuwa kupitia mfumo huo makini wa ushirikiano kati ya TASAF , CRDB pamoja na NIDA utaisaidia serikali kuwatambua wanufaika wanaolipwa kupitia mfuko wa TASAF na itapunguza mkanganyiko wa majina ya wanufaika wa mfuko huo kwani hapo awali changamoto ya majina ilitatiza wanufaika kupata fedha zao kutoka mfuko huo.
Aidha amewasihi wanufaika wa mfuko wa TASAF wahakikishe majina yao wanayoyasajili katika mfuko huo yaendane na yale yaliyoko katika vitambulisho vyao vya Taifa NIDA ili kuondoa changamoto za kujipenyeza Kwa watu wasio raia wa Tanzania ambao kwa kutokuwa waaminifu hutaka kujipenyeza ili kutaka kupata fedha hizo jambo ambalo limeanza kudhibitkiwa ipasavyo Kwa sasa
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bunda Bi, Jackline Maili amesema kuwa mpango wa TASAF wa awamu ya 3 kipindi cha II ambao umeanza kutekelezwa umewafikia zaidi ya walengwa 3198 ambao wananufaika na mpango huo ambapo 2604 kati yao hulipwa malipo ya fedha taslimu huku 594 wakilipwa kwa njia ya mtandao (E. Payments).
Amewashauri walengwa wote kujiunga na mpango huo kupitia benki ya CRDB ili wanufaika hao wasajiliwe na kupata fedha zao kwa wakati kupitia mtandao kwani ushirikiano wa Halmashauri ya mji ya Bunda, CRDB na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa, NIDA unaleta ufanisi na tija katika zoezi hilo.
0 Comments