Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM Z'BAR YAIPONGEZA ZIPA.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara yas Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Khamis Mbeto Khamis(kushoto),Mkurugenzi Mtendaji wa kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) Ndg.Shariff Ali Shariff (kulia) wakiziungumza juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mamlaka hiyo.
MKURUGENZI Mtendaji wa kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) Ndg.Shariff Ali Shariff (kulia),akimuonyesha picha maalum za visiwa vya Zanzibar vilivyokodishwa kwa wawekezaji Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara yas Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Khamis Mbeto Khamis(kushoto).


***********************
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.



CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema kimeridhishwa na
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika eneo la uwekezaji
kupitia Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar(ZIPA).

Kauli hiyo ameitoa jana Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM
Zanzibar Khamis Mbeto Khamis mara baada ya kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mtendaji ZIPA,Shariff Ali Shariff ofisini kwake Maruhubi.

Alisema ZIPA imetekeleza kwa kiasi kikubwa azma ya Rais wa wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ya
kuwavutia wawekezaji ambapo miradi mingi tayari imekwishawekezwa kwa
kipindi kifupi.

"Eneo la uwekezaji ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar hivyo
niwapongeze ZIPA kwa kazi nzuri mnayoifanya
na kasi kubwa mnayoitekeleza ya ilani ya chama chetu,"alisema

Katibu huyo aliitaka ZIPA kuendelea kufanya kazi kwa karibu na CCM
ili kufikia malengo ya ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo
wazanzibari.

Naye, Mkurugenzi wa ZIPA Sharif Ali Sharif, alisema, mwekezaji
anapotaka kuwekeza anapewa masharti kwa kuhakikisha anazingatia
mazingira ya uwekezaji yenyewe.

Alisema kwa sasa ZIPA imekuwa na uwekezaji wa miradi mikubwa 226
ambayo inaweza kuzalisha dola za kimarekani bilioni 3.5 ambapo
inatengeneza ajira zaidi ya 13000.

"Katika kipindi cha miaka hii miwili ya serikali ya awamu ya nane ZIPA
kupitia serikali tumetekeleza ilani kwa vitendo jambo ambalo
imeonyesha dhamira kwa serikali kuhakikisha uchumi
unaongezeka,"alisema

Alisema katika kipindi cha miaka miwili wawekezaji wameongezeka
kutokana na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Rais, Dk. Mwinyi
kutokana na kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji.

"Rais Dk.Mwinyi ameiimarisha ZIPA kiutendaji kwani Mamlaka hii imekuwa
na watendaji wenye uwezo mkubwa wa kitaalamu katika kuwavutia
wawekezaji na pia wameweka sheria ambayo ni rafiki zaidi kwa
wawekezaji,"alisema

Alisema kupitia miradi hiyo zimepatikana ajira mbalimbali kwa wananchi
wa Zanzibar na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha uchumi wa
unaongezeka kwa asilimia kubwa.

Pia, alisema uwekezaji umeongezeka kutokana na serikali kuanzisha
kituo cha pamoja ambacho kinatoa huduma zote kwa wakati mmoja ambapo
wawekezaji wamekuwa wakirahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa
wakati.

Akizungumzia upande wa visiwa, Mkurugenzi Sharif, alisema, kibali
kinachotolewa kwa muwekezaji hupewa masharti ya asilimia 10 ya eneo
husika na asilimia iliyobakia hupewa masharti ya kujenga ndani ya eneo
la baharini ili kuona visiwa hivyo havihathiriki na uwekezaji huo.

Mkurugenzi huyo alisema katika uwekezaji huo,muwekezaji utanguliza
fedha kabla ya kuwekeza ambapo kwa sasa serikali imeshaingiza dola za
kimarekani milioni 14 ambapo katika miradi ya visiwa hivyo inatakiwa
kuingiza dola za kimarekani milioni 19.

"Wawekezaji hawa wamekuwa wakilipa kwa awamu na fedha zilizoingia zipo
na zitatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kulipwa fidia watu
waliokuwepo katika bahari ikiwemo wavuvi, na wawekezaji ambao
hawakufikia vigezo tunavyovitaka," alisema

Akizungumzia suala la viwanda ndani ya visiwa vidogo alisema, katika
uwekezaji huo kutotakiwa uwekezaji wa viwanda vikubwa na kwamba
viwanda vinavyotakiwa ni vya kati na vyepesi ambavyo vitakuwa na
thamani kubwa.

Mbali na hilo,alisema ZIPA itaendelea kutekeleza ilani ya CCM katika
utendaji wao wa kazi wa kila siku na kufuata miongozo ya Rais
Dk.Mwinyi juu ya uwekezaji nchini.

Post a Comment

0 Comments