Ticker

6/recent/ticker-posts

BMH, BOMBO KUENDESHA KAMBI YA HUDUMA MBALIMBALI ZA KIBINGWA JIJINI TANGA


Na Oscar Assenga, Tanga

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) ikishirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo wanatarajia kufanya kambi ya huduma mbalimbali za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kuanzia February 27 hadi Machi 3 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Naima Yusuf (Pichani) alisema kwamba maandalizi ya kuelekea kambi hizo yanaendelea vizuri huku akieleza huduma za kibingwa zitakazotolewa.

Dkt Naima alisema huduma zitakazotolewa ni Upasuaji Mishipa ya Fahamu ,Mifupa, Mfumo wa Haja ndogo (Mkojo),Magonjwa ya ndani,Tiba ya Figo,Tiba ya Moyo kwa watoto na watu wazima.

Alizitaja huduma nyengine zitakazotolewa ni Magonjwa ya watoto Magonjwa ya macho,Tiba ya Kinywa na Meno pamoja na Magonjwa ya Uzazi kwa akina Mama.

Hata hivyo Dkt Naima alisema kwamba katika kambi hiyo wateja wa bima ambao watapokelwa ni wa Jubilee Insurance,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Assemble Insurance na Strategis Insurance.

.

Post a Comment

0 Comments