Mgodi wa Barrick wa North Mara, umekuwa mwenyeji wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Kampuni na Taasisi Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ngazi ya Taifa kilichofanyika kwa mara ya kwanza mkoani Mara.
Kikao kilifunguliwa na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jan Jacobs, ambaye alieleza kuwa kampuni inayo program ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanaimarisha afya zao kupitia michezo na mazoezi.
Mwenyekiti wa SHIMMUTA Taifa, Roselyne Massam ambaye aliongoza kikao hicho alisema kuwa lengo la kukutana ni kuweka mikakati, kufanya tathmini ya mashindano ya michezo mbalimbali yatakayoendeshwa na shirikisho hilo, lakini pia kuamua yafanyike lini na wapi mwaka huu.
“Tunaishukuru Barrick kama mwanachama na mdau wetu wa SHIMMUTA kukubali ombi letu la kuja kufanya kikao hiki hapa, hakika kikao kimekuwa cha mafanikio,” alisema Roselyne Massam.
Katibu wa SHIMMUTA Taifa, Dkt. Maswet Crescent Masinda, alisema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa, na maagizo ya Mlezi wa SHIMMUTA ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Philip Mpango, yanayolitaka shirikisho hilo kuhakikisha kuwa linawafikia wadau wake kuhamasisha ushiriki wa watumishi katika michezo.
Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Emmanuel Msaki, alisema kuwa kampuni imejipanga kushiriki mashindano ya mwaka huu“Hatukuweza kushiriki mashindano ya SHIMMUTA kwa miaka mitatu iliyopita kutokana na mlipuko wa corona uliokuwepo, ila niwahakikishie kuwa tutakuwa pamoja kwani kwenye bajeti zetu mwaka huu tumeweka na ya kutuwezesha kushiriki,” Msaki ameiambia Kamati hiyo.
Naye Meneja Usalama na Afya Mahali pa Kazi wa mgodi wa North Mara, Dkt Nicholas Mboya - katika kukazia kauli ya Msaki, amesema “Mwaka huu tunarudi kuwa sehemu ya familia ya SHIMMUTA kwa maana ya kushiriki kwenye michezo
Wajumbe Kamati hiyo ya SHIMMUTA pia walipata fursa ya kutembelea mgodi huo ikiwemo miradi ya kijamii inayotekelezwa na kampuni katika vijiji vinavyopakana na Mgodi huo.
Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara
Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara
Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya SHIMMUTA Taifa na wafanyakazi wa Barrick North Mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara.
0 Comments