Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro Issa (kulia) akizungumza katika moja ya mikutano iliyofanyika mkoani hapa. Kushoto kwake ni Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally.
Na Dotto Mwaibale, Singida
BARAZA Kuu La Waislam Tanzania (BAKWATA) , Mkoa wa Singida limelaani vikali na kupinga tabia ya baadhi ya watu ya kumdhalilisha Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally.
Akizungimza kwa niaba ya Bakwata na waislamu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro Issa alisema jambo hilo halivumiliki hata kidogo na kuwataka waliofanya hivyo kuacha mara moja, kwani Mufti ni kiongozi Mkuu wa Dini ya Kiislamu nchini na kama kulikuwa na jambo lolote dhidi yake wangeenda kumuona badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.
Hatuta kubali kuona watu wote wanaoingilia utendaji kazi wa Bakwata na kumdhalilisha Mufti kwa kauli za kejeli kama ilivyotokea hivi karibuni ambapo Muadhiri mmoja akimtaka ajipime.
“ Jambo hilo sio nzuri hata kidogo ebu tujipime mapema mwaka jana Mufti wa Tanzania alikuwa Misri ambapo chuo kimoja kikubwa kilimtunuku Tuzo ya heshima ambapo pia alifanya mambo mengi kwa ajili ya waislam halikadharika na Kenya pia walimtunuku tuzo kama hiyo sasa kiongozi wa namna hii kwanini adhalilishwe” alisema Sheikh Nassoro.
Alisema kuambiwa Mufti ajipe Bakwata Singida inaona wanaosema hivyo wamelenga kuleta machafuko hapa nchini na kutaka kumdhalilisha Mufti na kumshusha hadhi yake.
Alisema kitendo hicho wanakipinga kwa nguvu zao zote kwani Mufti anatosha kuwa kiongozi na ndio maana dunia nzima inamtambua na wametoa angalizo kuwa sio kila mtu anaweza kuwa msemaji na kuwa wapoviongozi wenye mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya waislam.
Nassoro alisema ifike wakati wa kuchunga mipaka ya kinidhamu waliopewa wanadamu hivyo hawatapenda kuona watu wachache wakijitokeza na kuanza kushambulia masheikh na Mufti.
Sheikh Nassoro ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali iwaangalie kwa kina watu wanaotumia nafasi ambazo sio zao kwa kutaka kuchafua hali ya utulivu na amani uliopo katika nchi yetu.
0 Comments