******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya yanga imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi kuu tanzania bara baada ya kufanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya Ruvu Shooting kwa kuichapa bao 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Ruvu Shooting walijifunga kupitia kwa beki wao wa pembeni Mpoki Mwakinyuke akijaribu kuokoa hatari mbele ya mshambuliaji wa yanga Kenneth Musonda na kutinga moja kwa moja wavuni.
Yanga Sc imeendelea kuwakosa wachezaji wao kadhaa akiwemo Nkane, Aucho, Morrison na Mshery ambao wamekosekana kwa sababu tofauti tofauti.
0 Comments