****************************
Mkuu wa mkoa kagera mhe Albert John Chalamila awesasisitiza wakuu wa wilaya kusoma na kuuelewa muongozo ili kuwarahisishia kujua na kuelewa mipaka yao ya kazi na kuepusha migogoro baina ya viongozi na viongozi.
Amesema hayo leo wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni na mhe Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa Mkoa kagera upo katika jitihada za kukuza uchumi wa mkoa na mtu mmoja mmoja , kuondoa changamoto za migogoro ya ardhi,kukomesha wizi wa mifugo na kahawa pamoja na kuhamasisha watu kufanya kazi kwa bidii na kutokomeza uvivu .
"Mikakati yote hiyo itafanywa kwa ushirikiano wenu nyinyi wakuu wa wilaya ndio nguzo za wilaya fanya kazi kwa ushirikiano na bila kufitiniana kuonekana mmoja anaweza na mwingine hawezi amesema.
Chalamila."
Aidha amemuagiza katibu tawala wa mkoa kuhakikisha anawarudisha kazini watumishi waliosimamishwa na kufukuzwa kazi bila sababu za msingi .
"Kuna taarifa za kuwafukuza kazi watumishi bila sababu za msingi: mfano, boss anamtongoza mfanyakazi akimkataa hana kazi na pengine akiona kumfukuza hawezi basi anamuhamisha kwa kumukomoa tusiishi kwa ufitina kiasi hicho.amesema Chalamila"
Pia amemuagiza kamanda wa police Mkoa Kagera kuhakikisha anawakamata watu wote wanaoshiriki kuwaozesha wanafunzi ikiwemo wazazi na baadhi ya viongozi wa serikali katika ngazi za chini pia na wale wanaoshiriki kuiba mifugo ya wananchi .
Hivi karibuni mhe dk Samia Suluhu Hassan aliwateua bw Aber Mwendawile kuwa mkuu wa wilaya Muleba, bw Jurius Karanga Raizer mkuu wa wilaya karagwe na bw Erastor Yohana Sima mkuu wa wilaya Bukoba na wote wamehapishwa loe.
0 Comments