Ticker

6/recent/ticker-posts

VYAMA VYA SIASA RUKHSA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA - SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini mara baada ya kuitisha kikao hicho kujadili masula ya kisiasa leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini mara baada ya kuitisha kikao hicho kujadili masula ya kisiasa leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akizungumza katika kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi akizungumza katika kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini wakifuatilia kikao cha Rais Samia Suluhu kilichofanyika leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe.Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba wakati wa kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.Freeman Mbowe akimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw.John Mnyika wakati wa kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe.Daniel Chongolo akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wakati wa kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakati wa kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.Freeman Mbowe akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bw. Hashim Rungwe katika kikao cha Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja Wenyeviti wa Vyama vya sisa mbalimbali mara baada ya kufanya kikao na viongozi hao leo Januari 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya adhara ya Kisiasa kufanyika na kufuata kanuni na sheria pindi mikutano hiyo inapofanyika.

Ametoa ruhusu hiyo leo Januari 3,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na viongozi wa kisiasa nchini ambapo amewataka kuacha siasa za matusi bali wakosoe pale wanapoona kuna mapungufu yamejitokeza.

Aidha amesema kumekuwa na siasa za kutukana baadhi ya viongozi walioko madarakani ambapo ni kosa na nikinyume na maadili ya nchi yetu hivyo waendelee kukosoa pale Serikali inapokuwa imekosea.

Amesema ni vizuri kwa vyama vingine kutoa mtazamo wao pale Serikali inapokuwa imejisahau ili iweze kutekeleza jambo hilo ili kuweza kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inafanya kitu.

"Siwezi kuwaita ni wapinzani, kwamaana sioni upinzani uliopo kwenye hili maana wakikosoa kitu ambacho hakichafanywa na Serikali, tunayachukua na kuyashughulikia ili Wananchi waone Serikali iliyopo madarakani inafanya kazi". Amesema Rais Samia.

Amesema kwenye maridhiano kati ya Chadema na CCM pamoja ya ripoti ya Kikosi Kazi masuala yaliyopendekezwa zaidi ni kuhusu kuruhusu mikutano ya kisiasa, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wakati huo huo, Rais Samia amesema Serikali inajiandaa kurekebisha Sheria anuai zikiwemo Sheria za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa ili kujenga taifa lenye umoja.

Rais Samia amesema ili taifa liwe moja lazima kuwe na maridhiano baina ya vyama vya siasa kwa lengo la kuendesha taifa lenye amani na utulivu kwa maendeleo ya taifa letu.

 

Post a Comment

0 Comments