Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega (kulia) akikabidhi fedha taslimu kwa Mkuu wa Kituo cha Children home Msimbazi Sr. Stella Xzavery, zilizotolewa pamoja na vitu mbalimbali Kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akiwajulia hali watoto wanaolelewa kituo cha Children home Msimbazi wakati alipotembelea kutoa msaada wa vitu vya zawadi ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega (kulia) akikabidhi vitu vya msaada Kwa niaba ya Rais Samia,kwa Masister (Sr) wa vituo vya Watoto vya Mburahati na Msimbazi katika kusheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
************************
Na Andrew Chale, Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 27 Januari, 2023, Kwa kutoa vitu mbalimbali katika vituo Saba (7) vya Watoto Yatima.
Vitu hivyo Saba vimekabidhiwa mapema leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega ambaye alimwakilisha Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo aliweza kukabidhi vitu na mbalimbali na fedha taslimu
Tukio hilo limefanyika katika Kituo Cha Children home Msimbazi Cha Ilala Jijini Dar es Salaam,
Ulega pia aliweza kukabidhi zawadi hizo kwa Kituo Cha Watoto Mburahati,
Katika tukio hilo, pia aliweza kutembelea na kujulia hali watoto hao …
[15:09, 1/27/2023] Andrew Chale: Rais Samia Suluhu Hassan Asherehekea Siku Yake Ya Kuzaliwa kwa kutoa msaada Kwa vituo Saba vya watoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 27 Januari, 2023, Kwa kutoa vitu mbalimbali katika vituo Saba (7) vya Watoto Yatima.
Vitu hivyo Saba vimekabidhiwa mapema leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega ambaye alimwakilisha Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo aliweza kukabidhi vitu na mbalimbali na fedha taslimu
Tukio hilo limefanyika katika Kituo Cha Children home Msimbazi Cha Ilala Jijini Dar es Salaam,
Ulega pia aliweza kukabidhi zawadi hizo kwa Kituo Cha Watoto Mburahati,
Katika tukio hilo, pia aliweza kutembelea na kujulia hali watoto hao wanaolelewa kituo hicho cha Msimbazi.
Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na pempasi za watoto, unga, Sabuni, sukari, maziwa,mafuta na vingine vingi.
Aidha, vituo vingine ambavyo vimepelekewa zawadi hizo ni pamoja: Vituo vya Tua ngoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza
0 Comments