Nabii na Mtume wa Kanisa la Bwana yesu kwa Mataifa yote lililopo Tabata Kinyerezi ,linalosimamia Taasisi hiyo Nabii Philibert Paschal akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
*************
Na Magrethy Katengu
Taasisi ya Philibert Paschal Foundation imelishauri Jeshila Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani kutowapa leseni Madereva wa pikipiki za kusafirisha abiria(Bodaboda) mpaka wapitiwe Mafunzo na vyuo vinavyotamvulikana ndani ya mwezi mmoja na kuendelea ili kisaidia jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za bodaboda zinazotokea mara kwa mara.
Akizungumza Jijini Dar es salaam na Waandishi wa habari Nabii na Mtume wa Kanisa la Bwana yesu kwa Mataifa yote lililopo Tabata Kinyerezi ,linalosimamia Taasisi hiyo Nabii Philibert Paschal amesema vijana wengi wamejiari kupitia Bodaboda lakini hawana Elimu ya kutosha juu ya matumizi ya chombo cha moto hiko kwani wakipatiwa Elimu hiyo inasaidia kuwafanya Madereva wa pikipiki za kusafirisha abiria ( Bodaboda) kuheshimu kazi yao nakufuata sheria za usalama Barabarani.
"Sisi kama taasisi tunashauri ufike wakati sasa Serikali iweke masharti ya Madereva bodaboda wasome kwenye vyuo vya Usafirishaji mfano NIT na wawekewe kigezo katika kupatiwa leseni lazima dereva awe amesomea udereva hata kwa kiwango cha cheti ndo apewe leseni hali hiyo itapunguza ajali za barabarani" amesema Nabii na Mtume Philibert Paschal.
Aidha amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Jeshi la polisi Kikosi Cha usalama Barabarani kutoa Elimu hiyo kwa Madereva bodaboda huku wakitembea na kauli mbiu isemayo "Linda bodaboda na abiria wake"hatua ambayo inawafanya Madereva hao kubadilika na kuheshimu kazi wanayoifanya kwani ndio inayowapatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Taasisi ya Philibert Paschal Foundation iliyoanzishwa mwaka 2021 imekua ikijihusisha na shughuli mbalimbali za Kijamii kwa kusaidia makundi Maalumu ikiwemo kundi la Wazee wasiojiw eza,Watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ikiwa ni sehemu yakuonyesha upendo pamoja na kuhakikisha makundi hayo yanapata mahitaji muhimu ya kibinadamu kama malazi
"Kwa mwaka huu 2023 mwaka Jana tuligundua kuna watoto wanaishi katika mazingira magumu huku wakiwa na mzazi mmoja na akitokea ameugua kushindwa kumudu gharama za matibabu hivyo kile Mungu atakachotubariki hatuwezi kufikia kila mtu ila tutatoa msaada wa kuwakatia bima za afya na kuwalipia ada za shule Watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu,pia wazee wasiojiweza nao tunajaribu kuwasaidia kuhakikisha nao wanapata mahitaji muhimu ,hivyo tunaomba wadau mbalimbali waweze kujitokeza kushirikiana nasi katika kufanikisha kufikia lengo haya" amesema Nabii
Hata hivyo Nabii na Mtume Philibert Paschal amesema Taasisi hiyo ina malengo ya kuwafikia watu wengi wenye mahitaji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es salaam na Mikoa mingine lakini kwa sasa Taasisi hiyo inakumbwa na changamoto ya kukosa rasilimali fedha huku mahitaji yakutoa msaada yakiwa ni mengi,hali ambayo pia imefanya kushindwa kuyafikia makundi yote Kwa mwaka 2022.
Aidha Kiongozi huyo wa Dini ametoa wito kwa viongozi wenzake wa dini kupendana na kuacha kutendeana vitu ambavyo vinawafanya waonekane ni Watumishi wa shetani nakwamba viongozi hao ndio wanawajibu wa kulinda amani nasio kupandikiza chuki kati yao.
0 Comments