Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo akizungumza na Wanachama na Viongozi wa CCM Tawi la Kibaoni Kata Ya Melela,katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM na Kusikiliza Kero Mbalimbali za wananchi Mkoa wa Morogoro, leo Januari 29, 2023
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo, akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la kibaoni kata ya Melela katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM na Kusikiliza Kero Mbalimbali za wananchi Mkoa wa Morogoro, leo Januari 29, 2023
Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Mjema akizungumza na Wanachama na Viongozi wa CCM Tawi la Kibaoni Kata Ya Melela,katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM na Kusikiliza Kero Mbalimbali za wananchi Mkoa wa Morogoro, leo Januari 29, 2023
********************************
Na Mwandishi wetu, Mvomero
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amewataka viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo wanayoyasimamia kiutawala huku akitumia nafasi hiyo lengo la Chama hicho na Serikali kwa ujumla ni kuona changamoto za wananchi zinapatiwa majawabu.
Akizungumza leo na wananchi pamoja na Wana CCM akiwa katika Kata ya Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro Chongolo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa katika kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi kwenye maeneo husika huku akieleza changamoto kubwa kwenye wilaya ya Mvomero ni migogoro ya ardhi.
“Mimi na wenzangu tumekuja Mvomero kwa ajili ya kuzungumza na wananchi, kusalimiana na kusikiliza changamoto zao.Nimekuja kuhangaika na changamoto za wananchi sio kupiga hadithi, nimepewa changamoto ya migogoro ya ardhi kati ya kijiji na kijiji, Kata na Kata na maeneo ya kiutawala. Changamoto hizi mara nyingi zinasababisha na viongozi ambao wanaongeza maeneo ili kupata kura na baadae anaacha kero kwa wananchi.
“Wakati mwingine inasababishwa na maslahi ya maeneo unaona upande huu wameshamaliza ardhi yao wanataka kukata eneo la wenzao kuhamia kule ili kujinufaisha na mara nyingine ni kwa ajili ya tamaa ya kuuza mashamba, tamaa ya malisho, tamaa ya kulima , na tama zinazoendana na hizo.
“Sisi viongozi ndio wenye jukumu la kutatua changamoto , viongozi tukinyooka na tukasimamia na sheria ya nchi iko wazi kwasaabbu hakuna kijiji kisicho na mpaka kwani yote imeanishwa , ukiona kuna shida ya kijiji na kijiji uje viongozi wenyewe ndio wanashida.Nimeona nianze na hilo kwasababu Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi.”
Chongolo amesema ni lazima viongozi wakate shauri,waamue kwa mioyo yao kwamba wanakwenda kumaliza changamoto ambazo hazina haja ya kulelewa kwa muda mrefu, changamoto ya mipaka kati ya kiutawala iwe ngazi ya kijiji, ngazi ya kata , ngazi ya wilaya ngazi ya mkoa , hilo linawezekana kama viongozi watakubali na ukiona kiongozi anavutia upande wake mara nyingine warejee yaliyofanywa na wazee huko nyuma.
Aidha amesema kumekuwepo na utataribu wa kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa ajili ya makazi, kilimo na ugufaji bado kumekuwa kukiibuka changamoto akitolea mfano wakulima wakipewa eneo wanalima hao hao lakini mfugaji akipewa eneo la mifugo anaalika na wenzake baada ya miezi sita anahangaika kutafuta malisho.
“Tatizo la wafugaji akiambiwa tu hili ni eneo la wafugaji wanaalika wengine ukishaalika wenzio 10 kama eneo ulitengewa wewe ujue baada ya muda mfupi halitakutosha hivyo wanajikuta mifugo imejaa na hakuna malisho wanaanza kusogea kutafuta malisho, wakisogea wanakuta mkulima amelima na kinachofuata ni ukorofi.
“Sababu mkulima hajaalika wengine kuja kulima kwenye shamba lake lakini mfugaji amealika na wenzake, hii mialiko kuna wanaosaidia kuifanikisha , ng’ombe haruki kama njiwa , lazima atembee anakopita kuna viongozi na wanaona, hatuwezi viongozi tunakuja kila siku tunaambiwa mgogoro wa wakulima , mgogoro wa wafugaji.
“Pale kwenye Kijiji kuna kiongozi analipwa fedha ya Serikali kila mwezi na analipwa ili ahudumie wananchi sasa migogoro hii ipo na analipwa mshahara.Lazim turejee kwenye miiko ya uongozi, turejee sura halisi ya watendaji kuwajibika na ili wawajibike ni lazima waliopewa kazi ya kusimamia hizo kazi wasimame kwenye kutatua changamoto,”amesema Chongolo.
Amesisitiza kuwa hawawezi kuwa na viongozi wanaosababisha mgogoro kila siku siku lazima wafanye maamuzi na wasimamie wanayoyaamua, kiongozi mzuri ni yule aneyewaambia ukweli na auansimamia na unaleta matokeo chanya.
0 Comments