Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE SALIM AWAPA TAHADHARI WANAOZIMEZEA MATE FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

















“Hamtazila kizembe”


Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham amesema hatamfumbia macho mtu yoyote atakekuwa kikwazo cha kukwamisha mradi wowote unaosimamiwa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.


Mbunge salim ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa shule ya sekondari mwaya kata ya Ruaha kwa lengo la kuwaomba wananchi kujitolea kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ili iweze kukamilika kwa wakati na ianze kutoa huduma.


Mbunge Salim pia amesema kwa mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Rais Dkt.Samia Sulluhu Hassan jimbo la Ulanga limepata kiasi cha shilingi Milioni themanini na tisa laki moja na arobaini elfu kama fedha za mfuko wa jimbo (89,140,000/=) ikiwa ni fedha nyingi kupatiwa tangu aingie madarakani.


Mbunge salim amesema kiasi cha Mil 50 amekielekeza kukamilisha bweni la wasichana Shule ya sekondari mwaya kata ya ruaha kwa lengo la kupunguza mimba za utotoni na kuinua kiwango cha elimu katika jimbo la Ulanga.


Aidha Mbunge Salim amemtaka mhandisi wa halmashauri hiyo ndugu Amir Athumani kuhakikisha wanazitumia vyema fedha hizo na zinakamilisha mradi huo wa bweni kwa wakati bila kikwazo chochote ili watoto wa kike waanze kulitumia.


Mbali na mkutano huo mbuge salim pia amefanya ziara ya kukagua miradi yote iliyopata fedha za mfuko wa jimbo kwa mwaka 2021/22 ili kujiridhisha kama fedha hizo zimefanya kazi vyema kama ilivyoelekezwa na kamati ya mfuko wa jimbo katika vikao vyao.

Mbunge salim amemshukru Rais Dkt Samia sulluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka wilaya ya Ulanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya,elimu,miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments