Na Sheila Katikula,Mwanza
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa ,Freeman Mbowe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ifanyike baada ya kufungiwa kwa miaka saba.
Hayo ameyasema leo kwenye uzinduzi wa mkutano wakwanza wa hadhala uliofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Amesema wamekaa vikao mbalimbali na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutafuta maridhiano ya taifa la Tanzania, namshukuru kwa uvumilivu na kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa ifanyike nchini.
Amesema Rais ni msikivu kwani anatambua umuhimu kuwa na demokrasia kila mtu anapaswa kumuombea ili aweze kusimamia haki katika uongozi wake.
Mbowe amewataka wananchi wa vyama mbalimbali kuacha kujenga taifa lenye visasi na badala yake wajibizane kwa hoja kwani kufanya hivyo itakayosaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Naye Katibu Mkuu wa Baraza la wanawake (BAWACHA) Catherine Ruge, amesema miaka saba bila mikutano imekuwa ni chuo cha mafunzo kwao kwani kwa sasa wako tayari kuwasemea wananchi matatizo yao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA taifa,John Mnyika amesema mikutano itafanyika maeneo mbalimbali kwani ajenda kuu ni kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
"Mikutano yetu itakuwa na fursa ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kwani watu wataudha bidhaa mbalimbali na kujipatia kipato",amesema Mnyika.
0 Comments