Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUMIZI YA MAGARI YA UMEME KUSAIDIA KUPUNGUZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MATUMIZI ya Teknolojia ya usafiri wa nchi kavu kwa vyombo vya usafiri kutumia umeme unaweza kusaidia kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa kwenye miji inayoendelea na kupunguza kuhatarisha afya za wakazi wa miji.

Ameyasema hayo leo Januari 25,2023 Jijini Dar es Salaam katika Kongamano lililowakutanisha nchi 10 kutoka Afrika kupeana uzoefu kwenye suala zima la kuhakikisha wanapambana na uchafuzi wa hali ya hewa kwenye miji.

Amesema kuna vichavuzi vingi vya hali ya hewa ikiwemo viwanda vinavyotoa hewa chafu, uchomaji hovyo wa takataka lakini kwenye hilo kongamano wameegemea kujadili uchafuzi wa hali ya hewa kupitia magari.

"Magari yamekuwa yakiongezeka katika miji na sasa kwasababu ya maendeleo, watu wengi wanamagari na matokeo yake wakati mwingine unakuta uegeshaji wa magari unakuwa shida na hata hivyo magari mengi yanaingia kwenye miji yakiwa yameshatumika hivyo kutoa hewa ambazo kimisingi zinaathiri afya na zinachafua hali ya hewa na mazingira kwa ujumla". Amesema Dkt.Gwamaka.

Aidha Dkt.Gwamaka amesema Matumizi ya mabasi kama vile BRT inaenda kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa nchini hivyohivyo hata suala la upangilio wa barabara sehemu kubwa hazina sehemu ya kuendeshea baiskeli au kuvukia kwa watu waenda kwa miguu.

Pamoja na hayo Dkt.Gwamaka ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi wa BRT kwani ni mmoja wa majibu ya kupunguza matumizi ya magari mengi katika mji ambayo yanachafua hewa na kuhatarisha afya za wakazi wa miji.



Post a Comment

0 Comments