Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKONDO AONGOZA KIKAO CHA WATAALAM WA HAKI NA SHERIA WA SERIKALI GHANA




*************************


Na Lusajo Mwakabuku - WKS


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo anaongoza Kikao cha Dharura cha Saba cha Kamati ya Kitaalam ya Umoja wa Afrika cha Wataalam wa Sheria wa Serikali katika masuala ya haki na sheria kinachofanyika Accra nchini Ghana kilichoanza jana Tarehe 16 mpaka 19 Januari, 2023.

Mkutano huu una jukumu la kupitia, kuchambua na kuhakiki itifaki zitakazowasilishwa kwenye kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika Februari, 2023. Itifaki zinazoendelea kujadiliwa ni Itifaki ya Ushindani Afrika, Itifaki ya Haki za Miliki Ubunifu Afrika na Itifaki ya Uwekezaji Afrika.


Kamati hiyo ambayo ina ngazi ya Wataalam na ngazi ya Mawaziri, moja kati ya majukumu yake ni kuchambua na kupitisha Mikataba ya Kimataifa yote ambayo inawasilishwa kwa Wakuu wa Nchi kwa ajili ya kuridhiwa. Kwa upande wa Mawaziri, kamati hii inajumuisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu, Mawaziri wenye dhamana ya Haki za Binadamu, Katiba na Utawala wa Sheria au Mawaziri au mamlaka nyingine zilizoidhinishwa ipasavyo na Serikali za Wanachama Mataifa.


Kamati ya wataalam inajumuisha Wataalam kutoka Nchi Wanachama wanaohusika na sekta zinazohusiana na mauala masuala ya Haki na Sheria, ambayo mikutano yake hutangulia kabla ya mkutano wa ngazi ya Mawaziri.


Mwishoni mwa mwaka jana, Tanzania ilichaguliwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Haki na Sheria ya Umoja wa Afrika kwa kipindi cha miaka miwili kutoka 2022 hadi 2024.

Post a Comment

0 Comments