MASHABIKI wa ngumi mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushuhudia pambano la ngumi la kufungua mwaka 2023 wakati w mabondia Mustafa Doto kutoka Dar es Salaam atakapopambana na Said Mundi kutoka Tanga katika mnyukano wa round 10 kesho Januari 18, 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa leo, Promota maarufu nchini, Ali Mwazoa na ambaye pia mtayarishaji wa pambano hilo alieleza kutakuwa na mengine ya utangulizi 9.
Mapambano hayo yatakuwa kati ya Jay Jay atakayepambana na Peter Julius wakati Jonas Mtafya atapigana na Patrick Kimweri. Wengne ni Hamis Mwambashi dhdi ya Haji Juma, wote kutoka Tanga.
Mtoto wa bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla, Snake Junior atapambana na Ali Reli wote kutoka Tanga..
Haya ni mapambano ya utangulizi kwa ajili ya mabondia chipukizi kuelekea pambano kubwa la aina yake mkoani na nchini Tanzania kati ya mabondia wawili wanaogopwa, Ibrahim Classic atakayemkabili bondia mwenye mikwara na ngumi nzito, Ndondande Harmer, wa nchini Zimbabwe. Pambano hilo litakuwa la round 10.
Promota Mwazoa alitoa wito kwa mashabiki wa jijini Tanga na nje ya mkoa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mabambano hayo mawili yatakayofanyika 18 na 28 Januari ambayo yatautangaza mkoa katika fursa za biashara na ajira.
Pia Mwazoa aliahidi kuandaa mapambano mengine ya ngumi ambayo yatatoa zaidi fursa kwa vijana wanaochipukia katika ulingo wa michezo ya ngumi nchini.
0 Comments