Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa (Mb) akihutubia wakati wa Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kagera za kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Kata ya Ihanda Wilaya Karagwe Mkoa Kagera, tarehe 28 Januari 2023.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa (Mb) akipanda mti katika hospital ya wilaya Karagwe ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kagera za kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Kata ya Ihanda Wilaya Karagwe Mkoa Kagera, tarehe 28 Januari 2023.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walioshirikia katika Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kagera za kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Kata ya Ihanda Wilaya Karagwe Mkoa Kagera, tarehe 28 Januari 2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi CCM Mkoa wa Kagera, Bi. Alphonsina Barongo akiongea wakati wa Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kagera za kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Kata ya Ihanda Wilaya Karagwe Mkoa Kagera, tarehe 28 Januari 2023.
********************
Karagwe - Kagera
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa (Mb) ameitaka Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kuunga Mkono Kazi kubwa ya kupambana adui ujinga inayofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kila Mtoto aliyefikisha umri kuanza Shule apelekwe kuanza masomo.
Bashungwa ameyasema hayo leo Januari 28, 2023 katika sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kagera za kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Kata ya Ihanda Wilaya Karagwe Mkoa Kagera.
Bashungwa amesema moja ya Msingi na jukumu kubwa la Jumuiya ya Wazazi ya CCM ni kuhamasisha na kuendeleza elimu nchini ili kufuta adui ujinga na kusimamia maadili katika jamii.
Amesema Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi imeweka Mkazo mkubwa katika kuboresha utoaji elimu nchini ambapo imejenga shule za msingi kila Kijiji na Shule za Sekondari kila kata nchi nzima.
Bashungwa amesema katika utawala wa miaka miwili ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa miundombinu ya shule shikizi zaidi ya 3,000 na ujenzi wa madarasa zaidi ya 20,000 kwa awamu mbili.
Aidha, Bashungwa amesema pamoja na Juhudi za Serikali kuwesha utoaji wa elimu bure kuandia darasa la Awali mpaka Kidato cha sita lakini takwimu zinaonesha wanafunzi walioandikishwa na ambao wameanza masomo mpaka sasa bado ni wachache.
Bashungwa ametoa wito kwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kuishi misingi ya kuasisiwa kwa Jumuiya hiyo na kuondokana na hali ya unyonge ikiwa ni pamoja kusimamia elimu na maadili ya vijana katika Jamii yetu.
Awali, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kagera, Bi. Alphonsina Barongo amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo mkoani Kagera na kuwleza kuwa Jumuiya hiyo itakuwa mstali wa mbele kusimamia miradi hiyo.
Katika Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, Jumuiya ya wazazi mkoa Kagera imepanda miti katika hospitali ya wilaya Karagwe na Kuweka wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo wilaya Karagwe katika kata ya Ihanda.
0 Comments