Mtaalamu huyo wa Masuala ya Fedha Miradi na biashara kutoka nchini Uholanzi Bw.Ben Philipseni akizungumza na waandishi wa habari Januari 3, 2023 katika ofisi zao zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jatu PLC Mhandisi Zaipuna Yonah akizungumza na waandishi wa habari Januari 3, 2023 katika ofisi zao zilizopo Jijini Dar es Salaam.
***************
NA Magrethy Katengu
UONGOZI wa Jatu ukishirikiana na Bodi ya Wakurugenzi ya JATU PLC umepokea ugeni wa mtaalamu wa masuala ya fedha, miradi na bishara kutoka nchini Uholanzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa JATU PLC Mohammed Simbano amesema mtaalamu huyo atakuwepo nchini kwa kazi maalumu ya kusaidia kampuni kutengeneza mpango kazi mpya wa biashara itakayoendana na dira na maono ya kampuni.
“Ikiwa ni pamoja na kushauri namna ya kuboresha uongozi pamoja na kushauri juu ya mabadiliko yanayoendelea na namna ya changamoto zote zikiwemo madeni kwa kuirudisha kampuni kwenye biashara,” amesema Simabano.
Sombano ameeleza kuwa uongozi mpya kwa kushirikiana na bodi, Serikali na wabia mbalimbali tayari umeshabaini changamoto za msingi za kufanyiwa kazi.
Kwamba mgeni huyo aliyekuja kwa ushirikoano wa taasisi ya PUM Netherlands Senior experts ataungana na wataalamu wa masuala ya fedha na mitaji ambao ni Luzane Financing na InterCapital Advisory Services kwa kushirikiana na SSC Capital ambao kwa sasa wanafanya kazi ya kuiandalia kampuni mpango kazi mpya wa biashara.
Vile vile kushauri juu ya mabadiliko yanayoendelea na zaidi kukuza mtaji kwa ajili ya kumaliza madeni yote kwa kuketi chini na wadai na kuona namna ya kuendesha miradi iliyokuwepo na kuisimamia kwa weledi na ujuzi ili kuleta tija na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zilizojitokeza.
“Pamoja nao kampuni itashirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ambao ni wanahisa, wakulima, washauri taasisi za Serikali na wahisani ili kuweza kukamilisha mchakato wa zoezi la kuleta mabadiliko katika kampuni,” ameeleza Simbano.
Amesema lengo la uongozi mpya ni kuhakikisha maono na malengo ya kuanzishwa kwa kampuni yanatimia
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jatu PLC Mhandisi Zaipuna Yonah amesema wataendelea kushirikiana na Serikali Ili kampuni hiyo iendelee kunufaisha wanaowekeza hisa zao za wanufauke na Kilimo Ili wajikwamue na Umasikini hivyo Mtaalamu huyo amekuja kwa wakati Muafaka
Neye Mtaalamu huyo wa Masuala ya Fedha Miradi na biashara kutoka nchini Uholanzi Ben Philipseni amesema ametokea kwenye taasisi waliostaafu hivyo Seikali yao haiwaachi wanawatumia kutoa ushauri hivyo Jatu ameangalia mfumo wa Jatu hivyo mfumo huo ukisimamiwa vizuri utaishi na utatoa matunda mazuri hivyo ataandaa mpango mkakati utakaoleta mafaniko makubwa.
0 Comments