Ticker

6/recent/ticker-posts

IGP WAMBURA AWATAKA POLISI WANAWAKE KUONYESHA MABADILIKO YA KIUTENDAJI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura (kushoto) akipokea katiba ya watendaji wa mtandao wa Polisi wanawake nchini TPF-NET kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao huo ambaye pia ni Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Susan Kaganda baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa mtandao huo kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 05 Januari 2023. Picha na Jeshi la Polisi.

********************

05 Januari 2023 Dodoma

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amewataka watendaji wa mtandao wa Polisi wanawake nchini (TPF- NET) kuonyesha mabadiliko ya kiutendaji hususani kwenye suala la uongozi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kazi za kipolisi.

IGP Wambura amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa mtandao huo kwenye kikao kilichowahusisha maafisa na askari wa kike wa vyeo mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF- NET) ambaye pia ni Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Susan Kaganda amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mtandao wa Polisi wanawake mwaka 2007 ambapo hadi sasa mtandao huo umefikia mafanikio mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto.

Post a Comment

0 Comments