Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
Naibu Rasi ,Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Christina Raphael,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Tafiti kwenye masuala ya Jinsia wakifatilia hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka akiwa pamoja na Mwakilishi wa Ubalozi Irish Bi.Mags Gaynar akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti masuala ya kijinsia mara baada ya kuzindua Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti masuala ya kijinsia mara baada ya kuzindua Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO
........................
Na Emmanuel Mbatilo-DAR ES SALAAM
CHUO Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimezindua Kituo cha Utafiti Masuala ya Kijinsia kwa Ufadhiri wa Ubalozi wa Irish kitakuwa na kazi ya kufundisha masuala ya kijinsiana na masuala ya tafiti za kijinsia pamoja na kufanya ushauri kwa mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya kijinsia.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Januari 19,2023 DUCE Jijini Dar es Salaam, Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka amesema Kituo hicho kinaenda kuwa sehemu ya tafiti mbalimbali za kijinsia zinakwenda kuratibiwa na na kinaenda kujenga uwezo wa watafiti mbalimbali nchini.
"Kituo hiki kinaenda kutoa uwezo wa namna ambavyo hata Serikali na mashirika mengine yanaweza kwenda kuangalia namna wanvyoweza kuyaingiza masuala ya usawa wa kijinsia kwenye mipango yao, sera zao na hata kwenye mambo mbalimbali ili kuweza kuhakikisha kwamba kila tunachokifanya tunaweka usawa wa kijinsia mbele". Amesema
Amesema wanafunzi watakuwa ni sehemu ya kituo hiki kwani wataanza kujengewa uwezo kuhusiana na namna ambavyo wanaweza kufanya utafiti kuhusiana na masuala ya kijinsia lakini pia Vyuo Vikuu huwa wanawashirikisha wanafunzi katika kufanya tafiti hivyo watawahimiza wanafunzi kufanya tafiti zinazohusiana na masualaya kijinsia.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw.Yohana Sekimweli ameshauri vyuo vingine kuona Chuo cha DUCE kama mfano kuanzisha vituo vya utafiti kwenye masuala ya kijinsia ili kuweza kulikomboa taifa linafikia kwenye usawa wa kijinsia wa hamsini kwa hamsini.
Amesema mpaka kumekuwa na uwanzilishwaji wa madawati ya kijinsia kwenye maeneo mbalimbali hivyo basi kuanzishwa kwa vituo kama hivi vitasaidia kupunguza mauala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye taifa letu na baadae kuweza kuondokana na masuala kama haya.
Nae Mratibu wa Kituo cha Utafiti Masuala ya Kijinsia DUCE Dkt.Cresencia Massawe amesema kundi la walimu ni muhimu katika kufikisha uelewa wa masuala ya kijinsia na kueleta mabadiliko makubwa endapo wakiivishwa kwenye masuala ya kijinsia .
0 Comments