Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.( Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Hafidh)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiungana na wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kiwani katika kuimba wimbo wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kufungua Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na watoa huduma katika Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kufungua kituo hicho leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiagana na wananchi wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kufungua Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
*************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha miundombinu ya afya kwa kufanya matengenezo na kujenga miundombinu ya kisasa na kusogeza huduma ya afya karibu na wananchi huku mfumo wa rufaa ukiboreshwa zaidi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Kituo cha Afya Daraja la Pili cha Kendwa kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 10 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Amesema serikali ipo katika hatua za mwisho kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kupitia Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar pamoja na uwepo wa mipango mahususi ya kuongeza idadi ya wafanyakazi wa afya katika vituo vya afya na hospitali na kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kikamilifu na kwa wakati.
Makamu wa Rais ameupongeza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) kwa kuweza kushirikiana vyema na Serikali katika kuunga mkono juhudi za kuimarisha na kusogeza karibu na wananchi huduma za kijamii ikiwemo ujenzi huo wa kituo cha Afya Kendwa kilichogharimu shilingi milioni 527.
Amesema kituo hicho kitaweza kuhudumia Shehia ya Kendwa,Kiwani, Mtangani na Shehia nyingine za jirani na kuwezesha wananchi kupata huduma bora za matibabu ikiwa ni pamoja na huduma za mama na mtoto, maabara na huduma za chanjo pamoja na kusaidia kuwapunguzia wananchi hususan kinamama wajawazito kutembea masafa marefu kufuata huduma za Afya.
Aidha Makamu wa Rais ametoa Rai kwa wananchi pamoja na watoa huduma katika kituo hicho kutunza vyema majengo na vifaa vilivyomo na vitakavyonunuliwa.
Amewasihi watumishi watakaopata nafasi ya kuishi kwenye nyumba za madaktari, kuzitunza vizuri nyumba hizo ili kuepusha gharama za matengenezo yasiyo ya lazima na kuwakumbusha viongozi wa Kituo hicho kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanapanda miti katika eneo la Kituo pamoja na makazi ya madaktari na kutunza na kupendezesha mazingira yake kwa kuyaweka safi.
Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Afya, madaktari na wahudumu wa afya kuongeza jitihada za kutoa elimu ya afya hususani ile inayolenga katika kuwakinga watanzania na magonjwa ya kuambukiza na hata yasiyoambukiza ili kuepuka gharama kubwa za matibabu.
Amewasihi kuwa wabunifu katika kutoa elimu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, teknolojia ya Habari na mawasiliano pamoja na mifumo ya kidigitali.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Wizara itaendelea kuhakikisha huduma zinazotolewa katika sekta ya afya zinaendana na wakati ikiwemo kuongeza vifaa mbalimbali vya kisasa katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
Ameongeza kwamba kwa sasa Wizara inalenga kuwashirikisha wananchi katika kusimamia vituo hivyo ili viweze kuleta tija ikiwemo kuondoa uzembe na ubadhirifu wakati wa utoaji huduma.
0 Comments