Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wanachama wa CCM Shina Namba 18 Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabib alipowasili katika ziara ya siku 9 mkoani Morogoro, yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na uimara wa chama, kuzungumza na wana-CCM pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wanachama wa CCM Shina Namba 18 Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu akizungumza na wanachama wa CCM Shina namba 18 Kata ya Itaragwe kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, katika ziara Ya Katibu Mkuu wa CCM ya Siku 9 mkoani Morogoro yenye lengo la Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Miradi ya Maendeleo, kuzungumza na Wana CCM pamoja na Makundi mbalimbali ya Wananchi.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema akizungumza na Wanachama wa CCM Shina namba 18 Kata ya Itaragwe kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, katika ziara Ya Katibu Mkuu wa CCM ya Siku 9 mkoani Morogoro yenye lengo la Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Miradi ya Maendeleo, kuzungumza na Wana CCM pamoja na Makundi mbalimbali ya Wananchi.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema, Akitembea pamoja na Vijana Wa Hamasa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kumaliza mkutano Wa Wanachama wa CCM Shina namba 18 Kata ya Itaragwe kitongoji cha Matale.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongolo, Akisukuma Chuma kinachoendesha mashine ya Kukamulia Juisi ya Miwa kwa ajili ya Utengenezaji wa Sukari Gulu inayozalishwa na Kikundi Cha Wanawake Cha Jitihada kilichopo kata ya Idiba Wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro,Akiwa katika Kikundi hicho Ameahidi kuwapatia Mashine Mpiya ya Kisasa ili kuongeza Utengenezaji wa Sukari Guru katika kikundi hicho
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongolo,akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Mkwajuni na Ilalo mara baada ya kujionea kero kubwa ya kukosekana kwa daraja katika mto Nguyamilinalounganisha vijiji hivyo viwili wilayani Gairo mkoa wa Morogoro.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongoloakisaini Kitabu Cha Wageni kwa Balozi wa Shina Namba 1 Katika Kijiji Cha Kidebya akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Organaizesheni Issa Haji Gavu Pamoja na Viongozi wa Chama Mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongolo akiwa pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe Ahmedi Shabibi wakati akikagua maendeleo ya Mradi wa Maji wa Serengeti Halmashauri ya Manispaa ya Gairo. (PICHA NA FAHADI SIRAJI CCM MAKAO MAKUU)
………………………………………….
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo amesema Dhamira ya Chama hicho ni kuendelea kutafuta Suluhu ya Changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi kwenye maeneo yao, ikiwemo ile ya Miundombinu, Elimu, Afya, Kilimo, Maji pamoja na Ardhi.
Komredi Daniel Chongolo ametoa kauli hiyo leo mkoani Morogoro wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya Gairo alipokuwa akianza ziara yake ya Kikazi ya Siku tisa katika mkoa huo.
Kuhusu migogoro ya Ardhi katibu mkuu huyo wa CCM amesema anatambua mkoa wa Morogoro unayo Changamoto kubwa ya Migogoro ya Ardhi ambayo inasababishwa na Baadhi ya Watu kutozingatia Suala la Mipaka ya maeneo na hivyo kuzusha migogoro isiyokuwa na tija kwa maendeleo yao.
“Kubwa kwenye mkoa huu ni Changamoto ya Migogoro ya Ardhi ambayo inatokana na Wakulima na Wafugaji ambayo huchochewa wakati mwingine na Watendaji wa Serikali, ambao Wanashindwa kutimiza wajibu wao” amesema Chongolo.
Kuhusu Suala la Maji, Chongolo amesema anatambua Wilaya hiyo inayo Changamoto ya Upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa eneo hilo, ambapo Serikali inaendelea na Jitihada za Kutatua tatizo la maji.
“Lengo la kuja hapa ni kuja kuangalia Changamoto za mkoa huu, tumekuja wakati huu ili kuangalia vyanzo vya maji, tunajua wengi wenu hapa mnatumia maji ya visima, mpango Uliopo ni kuangalia namna ya kutega maji kutoka milimani ili hatimae kuondokana na Changamoto ya maji” ameeleza Chongolo.
*Kwa Upande wake Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema* amesema Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuzunguuka nchi nzima kwa ajili ya Kusikiliza na Kutatua kero mbalimbali za Wananchi na kuzipatia Suluhu ya Kudumu kama ili kutumiza Dhamira njema ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwenye Ziara hiyo ameambatana na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu kwa ajili ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho pamoja na kuzungumza na Makundi mbalimbali.
0 Comments